Simba msikurupuke Victorien Adebayor ameshuka kiwango

ngara23

JF-Expert Member
Joined
Aug 31, 2019
Posts
9,091
Reaction score
21,087
Salaam,

Viongozi wa Simba nawapa tahadhari tena msije kukurupuka kumsajili Victorien Adebayor raia wa Niger aliyeshuka kiwango sana

Mchezaji huyu amepoteza namba kwenye taifa dogo kimpira Niger
Ni miaka miwili yuko bench kutokana na kushuka kiwango toka alipohamia RS Berkane hawajawahi kucheza hata mchezo wa kirafiki

Na sasa yuko Amazulu akisuburia benchi na team ya Amazulu ina mpango wa kumwacha kama free agent

Za ndani ni kwamba week iliyopita alifika Dar es Salaam kusaini Simba
Simba wanaendelea kukurupuka kwenye usajili kama kawaida yao na wakipigwa 5G wataanza kulalama ati wachezaji wamerogwa

Scouting team ya Simba imelala hadi wameamua kusajili hili garasa Adebayor

5G itawakuta tena miaka 10 mfululizo hadi viongozi wenu watakapo pata akili
 
Shida simba hawajui scoutting walikua wanategemea sana yanga ipoint wakachukue kwanzia kina wawa chama kondeboy kagere manura nyoni boko nk
Adebayor wameangalia record ya miaka miwili nyuma
 
Simba viongozi wana matatizo, wanataka adebayor(winger wa kushoto) je simba ina shida ya winger,? Je mido haina shida, je wasaidizi wa kapombe na tshabalala wapo?
Chama langu siku hizi limekuwa la hovyo sana, mijitu iliyopo pale huenda haijui soka, ni mijitu ya kukurupuka.
Wanayoyafanya pale ni kama wanasiasa wa bongo tu, kupanda gari la milioni mia 4 ila akifika kwenu anapanda punda mjione mko nae sawa. 😂🤣
 
Makonda kakukosea nini
 
Simba nitawadharau sana wakimsajili Adebayor nitawaona wehu
 
Makonda kakukosea nini
Dah! Sijui uzee ndiyo unaniandama!! Maana nimejaribu kusoma maelezo ya jamaa, hakuna sehemu nimeona amemtaja huyo Makonda aka Daudi Albert Bashite; kijana kutoka Kijiji cha Koromije!!
 
Don't awake a sleeping man, if you do so, you will sleep yourself.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…