kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 13,778
- 14,214
Nimemsikia mtu mmoja akitoa hoja ya kushitaki mahakamani mabango yaliyowekwa na Yanga barabarani. Ukweli ni kwamba aliyeyaweka haya mabango inaitakia mema Simba kuliko huyu anaetaka mabango yapelekwe mahakamani; haitakii mema Simba,
Mabango ya Yanga yalipaswa kuisaidia Simba kutafuta wapi hasahasa walijikwaa na nini wafanye wasijikwae tena kwa namna ileile ya 1-5 siku zijazo. Huyu anaewaza kwenda mahakamani ni mufilisi na adui namba moja wa Simba anaecheza mpira mdomoni na kuuficha uhalisia kuwa Yanga ni bora zaidi wakati huu kuliko Simba wakati huu. Ubora wa Yanga unadhibitishwa na TFF, CAF na vyombo vingine vya mpira duniani.
Ubora wa Yanga wa sasa ulichagizwa na wachambuzi wengi (Jemedari, Jeff, na wengine) na wadau wengine wa mpira kuuponda ubora wa Yanga dhidi ya Simba. Wachambuzi wengi walikuwa wakiisifu mno simba kuliko Yanga bila kujua kwamba wanaisaidia Yanga indirectly kujiimarisha na kuibomoa Simba kwa kuipamba sana kupitiliza.
Wadau wa Yanga wanapaswa kumlaumu huyu anaeweka mabango ya kuikejeli Simba kupita kiasi kwakuwa kufanya hivyo Simba itaimarika sana kupitia kejeli hizi.
Badala ya Simba kuhangaika na kejeli za Yanga mahakamani wahangaike na Simba yao (ufundi, uongozi na wachezaji) ili kuepuka aibu, maana aibu ya kiwanjani itamalizwa kiwanjani hukohuko sio mitaani wala mahakamani. Kufanya hivyo ni sawa na mtu kukivunja kioo chake kwa kosa la kumuonyesha matongotongo yake machoni.