Simba na Vunja Bei wanamuogopa Manara kumbe GSM anatengeneza jezi za Simba

Simba na Vunja Bei wanamuogopa Manara kumbe GSM anatengeneza jezi za Simba

CHIZI VITABU

JF-Expert Member
Joined
Jun 12, 2021
Posts
1,061
Reaction score
2,477
Ukisikia aibu ni hizi kumbe kutwa nzima tunaiponda GSM na Manara anatucheka tu kimyakimya , wanasimba kwa pamoja tuwaombe radhi Gsm kwa mujibu wa clip ya manara instagram ni kwamba GSM ndiyo wanaotengeza jezi za simba hiyo ni baada ya kuonekana kilichoitwa jezi feki za simba

Ukiamini kwamba ni feki basi wewe ni mjinga maana siyo vunja bei wala klabu simba waliothubutu kusema lolote hadi sasa

MANARA OYEEE GSM OYEEE WABURUZENI MAFALA HAO KUMBE KELELE ZOTE ZILE NYIE NDO MNALTULETEA JEZI MJINI??

Inaelezwa watu kadha wamekamatwa kwa kukutwa na wako polisi kwa kosa la kuuza jezi Feki za Simba zenye nembo za Yanga na GSM. Ambayo sio washirika wa utengenezaji wa jezi hizo.

Lakini juzi kati Manara alipost video na kusema hata jezi za Simba zimetengenezwa na GSM ambazo ndio hizo jezi Feki sasa Manara anatakiwa kuthibitisha kauli yake ya hizo jezi zimetengenezwa na GSM ikiwa klabu ya Simba inawatafta waliotengeneza hizo jezi na kuziuza bila kibali kutoka Simba.

Kwa sasa Manara yupo nje ya nchi lakini pia hadi sasa GSM wala Yanga hakuna aliye toka na kukanusha kauli ya Manara.
 
Kama Vunja bei na GSM ni partner kibiashara kwa namna mbali mfano sub-contracting na etc ifahamike, na hili litaleta mwangaza wa faida au hasara za uzombi na uzuzu wa zeruzeru kwa Matopolo.
 
msemaji wa yanga kathibitisha kwenye account yake ya insta huna habari ndugu? Kumbe simba kelele nyingi gsm ndiye anawatengenezea jezi
Wewe ndiye huna update Vunjabei ameshasema suala hili wamewakabidhi wanasheria walishughulie au ulitaka wafuate staili ya mke wa Mzee Tozi kuropoka ropoka? Wewe endelea kumuamini huyo nyama mbichi wako
 
Sasa, kwa taarifa hii, SIMBA wapataje aibu, kama kwa mujibu wa thread yako hii, unasema GSM kumbe ndiyo watengenezao jezi fake za Simba na kuzimwaga mitaani?
 
msemaji wa yanga kathibitisha kwenye account yake ya insta huna habari ndugu? Kumbe simba kelele nyingi gsm ndiye anawatengenezea jezi
Tatizo liko wapi kwani, si anafanya biashara? Simba imelipwa hela sh. bilioni mbili na imemaliza kazi, ni juu ya mtengenezaji kujua namna gani atazirudisha hela zake, iwe kwa kutengeneza yeye au kwa kukodisha watengenezaji wngine. Mkiambiwa GSM ni Simba damu mnakuwa wabishi. Kwani kanisa linapojengwa haliwezi kuchukua mkandarasi. mafundi au vibarua waisilamu?
 
Nimejaribu kusoma ili nielewe ila bado bado. Iwapo nimekuelewa vizuri, basi unamaanisha kwamba Manara ametoa siri za bosi wake GSM kwamba yeye (GSM) ndiye anayetengeneza jezi feki za Simba. Sina uhakika kama umemaanisha hivyo au vinginevyo.

Kama ni hivyo, basi GSM ataingia matatani kwa kushtakiwa na Vunjabei, na mashahidi wa Vunjabei watakuwa ni Simba (waliouza haki kwa Vunjabei tu) na Manara (aliyetoa siri hiyo hadharani)
 
Vunjabei kajichomeka simba mwaka mbaya Sana. Hizi jezi hazitauzika tena
 
Nimejaribu kusoma ili nielewe ila bado bado. Iwapo nimekuelewa vizuri, basi unamaanisha kwamba Manara ametoa siri za bosi wake GSM kwamba yeye (GSM) ndiye anayetengeneza jezi feki za Simba. Sina uhakika kama umemaanisha hivyo au vinginevyo...
Mkuu, na mimi nimemuelewa hivyo huyu aliyeanzisha thread hii!
 
Back
Top Bottom