Simba na Yanga, hawa makocha wazawa kimataifa hawatufikishi popote

mpimamstaafu

JF-Expert Member
Joined
Jul 18, 2018
Posts
4,445
Reaction score
4,707
Hakika sikio la kufa halisikii dawa,

Tanzania bado ni kichwa cha mwendawazimu.Ukweli ulio wazo viwango vya Makocha wetu wazawa ni mdogo sana kwani January mpaka Desemba tupo nao hapa hapa hawajatoka kusema wamekwenda kupata Mafunzo na mbinu mbalimbali za mpira nje ya nchi kwenye Vyuo mbalimbali.

Vilabu vyetu vimekuwa vinashiriki kwenye mashindano ya kimataifa na vilabu vyenye uwezo mkubwa wa kuajiri Makocha wenye uwezo mkubwa matokeo yake ni kutolewa mapema. Nashauri viongozi wa vilabu vyetu kuwa hawa Makocha wazawa hawawezi kutuvusha Kimataifa tafuteni Makocha wenye ujuzi na elimu ya mpira.
 
Uwekezaji mdogo katika kuandaa vipaji hilo tu.
 
Makocha wazawa wanauwezo mkubwa tu wakutufikisha mbali endepo tu watawezeshwa katika masuala ya kiufundi na kuwa na benchi LA ufundi LA uhakika na vile vile wasiingiliwe kwenye maamuzi yao.
 
hao makocha wa kigeni si ndio wametimuliwa kwa kuchemsha kimataifa? wacha wazawa wachukue nafasi
 
Haji manara ni mpumbavu sana yan kocha aliyewapa mafanikio kias kile had kucheza robo fainali anaanza kumwongelea vbaya as if ashawah kuwa kocha ndo mana soka letu haliendelei kwa sababu tumeipa nafas akiki ndogo iongoze akili kubwa
 
Makocha wazawa wanauwezo mkubwa tu wakutufikisha mbali endepo tu watawezeshwa katika masuala ya kiufundi na kuwa na benchi LA ufundi LA uhakika na vile vile wasiingiliwe kwenye maamuzi yao.

Kocha wa kibongo Hata ukimpa milion 100 hakuna kitu atafanya zaid ya story tu za uongo uongo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…