Pre GE2025 Simba na Yanga hutumika kuzima vuguvugu au kusahaulisha wananchi changamoto zao za kijamii

Pre GE2025 Simba na Yanga hutumika kuzima vuguvugu au kusahaulisha wananchi changamoto zao za kijamii

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Mhaya

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2023
Posts
1,831
Reaction score
5,489
Katika nchi yetu ya Tanzania, kama ilivyo katika nchi nyingi nyingine, michezo, hasa mpira wa miguu, ina nguvu kubwa katika kuvutia na kuunganisha watu. Timu za mpira wa miguu kama Simba na Yanga huvuta umakini wa kitaifa na mara nyingi hata kimataifa. Vyombo vya habari na wananchi kwa ujumla huwekeza muda na hisia zao katika timu hizi, hivyo kupunguza umakini kwenye masuala mengine muhimu ya kisiasa au maendeleo.

Mpira wa miguu unaweza kutumika kusahaulisha wananchi kuhusu mambo ya kisiasa na maendeleo, hasa endapo kunakuwa na dalili za kuibuka kwa vuguvugu la wananchi kulalamikia au kutaka kuandamana au kugoma. Katika nchi ambazo michezo haijashika kasi au hisia kupita kiasi, kama Kenya, wananchi wanaweza kulalamikia kuhusu maendeleo yao au mambo ya kisiasa kwa sababu hakuna kitu kinachowafanya wasahau changamoto zao. Akili zao zote ziko chonjo kufuatilia mambo yanayohusu mustakabali wa maendeleo ya nchi yao, na ndio maana wanapoona mambo hayaeleweki kuhusu serikali yao husimama kidete na kutaka haki itendeke.

Hapa Tanzania ni tofauti kidogo. Mashabiki wengi wa mchezo wa mpira wa miguu ni vijana wenye umri mdogo mpaka kufikia uzee, zaidi ya 70% ya wananchi wote hushabikia Simba au Yanga. Ukizingatia kundi hili ni muhimu zaidi katika kujenga nchi, purukushani za michezo, hasa usajili na mechi kubwa kama hizi za Simba na Yanga, huleta umoja na shauku miongoni mwa wananchi kufuatilia matukio yanayoendelea katika timu hizi. Hii inaweza kusaidia kuhamisha mawazo yao kutoka kwenye malalamiko ya kisiasa na maendeleo na kuelekeza nguvu zao kwenye kushabikia timu zao. Hii inafanya watu kujihusisha zaidi na michezo kuliko kuangazia masuala mazito ya kisiasa au maendeleo.

Wakati kuna dalili za wananchi kulalamikia kwenye vijiwe vya kahawa au sehemu zozote zenye mikusanyiko mikubwa, serikali na vyombo vya habari vinaweza kutoa kipaumbele kwa matukio ya michezo ili kuepuka migogoro au kuenea habari muhimu za kisiasa au zinazohusu changamoto za kimaendeleo kwa wananchi. Endapo kutatokea malalamiko ya wananchi, vyombo vya habari na media za mtandaoni zinaweza kuelekeza umakini wao kwenye mechi, matukio makubwa ya timu au habari za Simba na Yanga ili kupunguza nafasi ya kuenea kwa habari za malalamiko. Hii inaweza kuwa mkakati wa makusudi wa kupunguza au kuzima mvutano wa kijamii na kisiasa kwa muda mfupi au mrefu kati ya wananchi na serikali yao.

Msemaji maarufu wa michezo, Haji Manara, aliwahi kudokeza kuhusu mbinu hizi za michezo kutumika kuzima hisia za wananchi kuhusu maendeleo yao. Tazama video hii kwa maelezo zaidi.

 

Attachments

  • VID-20240718-WA0000.mp4
    1.1 MB
Hao ndo watz,ila believe me,wanadam hubadarika sana, ipo siku tu.
 
Back
Top Bottom