Simba na Yanga jengeni viwanja vyenu ni aibu sasa

Nyamesocho

JF-Expert Member
Joined
May 5, 2023
Posts
487
Reaction score
1,287
Haya serikali imetangaza kufunga viwanja vya Benjamin Mkapa na Uhuru mpaka Oktoba 2024 ili kuvikarabati

Simba na Yanga wanatamba kila upande kuwa ni timu kubwa Afrika mpaka Duniani lakini cha kushangaza hazina viwanja angalau vya mashabiki elfu kumi na tano

Simba na Yanga ni aibu kutegemea viwanja vya serikali na timu ya Azam huku mkitamba nyinyi ni wakubwa Afrika na mnamashabiki wengi ndani na nje ya nchi hii ni aibu aisee

Msitusumbue na kelele na timu kubwa na huku hakuna hata viwanja

Shame on youuu , https://jamii.app/JFUserGuide you
 
Naunga mkono hoja. Mimi ni mmoja ya wadau wa michezo ambao huwa ninachukizwa sana kuona timu kongwe, kubwa, maarufu na zenye mashabiki wengi ndani na nje ya nchi; kukosa viwanja vyao binafsi.

Viongozi wengi wamekuwa wakivitumia hivi vilabu viwili kujinufaisha zaidi kiuchumi, na pia kisiasa!! Badala ya kuwekeza kwenye miundombinu.
 
Taifa lenyewe Lina kiwanja 1.tena kwa msaada.uwanjani ameendi,jezi hamnunui,ada za ya achana ziro.hizo fedha zinatoka wapi?za MO au GSM?.hivi mmewahi kufuatilia gharama za uendeshaji?mapato ya klabu,gharama za ujenzi wa uwanja angalau wa watu 20,000 waliokaa.
Watu wa dar wenye mdomo Sana ndio wanaongoza kutoingia mechi zao.labda iwe Simba vs Yanga,au hizo dhidi Azam.
Shirikini kwenye kuchangia mapato.
Yanga ikifikisha wanachama1,000,000 Kuna haku ya kudai uwanja na kuwajibisha viongozi wakifeli.
Tambueni UCHUMI wa klabu zenu .sio UCHUMI wa MO au GSM
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…