Simba na Yanga kuzomeana ni kawaida, hata kwa wenzetu uzalendo ni timu ya taifa

Simba na Yanga kuzomeana ni kawaida, hata kwa wenzetu uzalendo ni timu ya taifa

Aaron Arsenal

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2014
Posts
24,501
Reaction score
28,711
[emoji375]Uhasimu wa El Classico

Kwenye fainali ya Liverpool na Madrid msimu uliopita inasemekana baadhi ya mashabiki wa Barcelona walinunua jezi za Liverpool na kwenda kuishabikia Liverpool.
::
[emoji375]Uhasimu wa Liver na Man United
Kwenye mechi ya Barcelona na Liverpool katika jukwaa la Barcelona alionekana shabiki mmoja akiwa amevaa jezi ya Man United akiwashangilia Barca.
::
[emoji375]Waingereza wenyewe kwa wenyewe
.
Juzi Rio Ferdinand ameonakana akiwa na Gary Linekar wakishangilia bao la Messi tena kwenye moja ya vituo vikubwa vya Runinga nchini Uingereza cha BT Sports. Shabiki mmoja wa Liverpool akamwabia Linekar katika ukurasa wa twitter kuwa amejishusha heshima na sio mzalendo, Linekar akamjibu na kumwambia najua inauma, pole sana (kibongobongo ni kama alimwambia tulia dawa iingine.) kumbuka Linekar aliwahi kuichezea Barca.
::
[emoji375]PSG na Maadui zake

.
Katika mchezo wa PSG na United Evra na Eric Cantona walishangilia sana bao la Rashford bila kujali kama wao ni wafaransa. Hapo hapo kuna mashabiki wa Lyon walikuwa wamebeba bendera ya United wakiwa wamevaa jezi za Lyon.
::
[emoji375]Uhasimu wa Everton na Liverpool
.
Mwisho ambayo ndio funga kazi ni kilichotokea hivi leo, katika moja ya maduka ya mahasimu wakubwa wa Liverpool ambayo ni klabu ya Everton. Katika maduka hayo yameonakana yakiizua skafu za Lionel Messi. Yaan wameanza maandalizi ya kuwapokea Barca kwa mikono miwili.
::
Hili pia limenikumbusha kauli ya David Beckham alipowaomba Madrid iwafunge Liverpool.
::
Uswahili haujaanza hapa, upo kote duniani, kila mmoja apambanie mafanikio yake usitegemee sapoti kutoka kwa adui yako

KUTOKA KWA SHAFFIH DAUDA

shaffihdauda_-20190504-0001.jpeg
 
Kwenye masuala ya vilabu timu inapaswa kutengeneza fanbase yake siyo kutegemea adui zako wakusapoti unapocheza na adui yako mwingine wa nje. Kumbuka adui wa adui yako ni rafiki yako kwani adui yenu ni mmoja.

Njia ya kutengeneza fanbase ni kushinda tu hakuna namna kwani Azam walijizolea mashabiki wengi walipokua wanazifunga sana Simba na Yanga na kuchukua kombe, wangekua mbali sana kama wasingejikwaa walipojikwaa.

Unakumbuka Mbeya City kwenye ubora wao nadhani ni timu ambayo jezi zake zimevaliwa sana mtaani ukiacha Simba na Yanga,Sokoine ilikua inakua zambarau tupu uwanja unajaa ila leo hii siyo hivyo tena.

Yanga walikua wengi sana uwanjani kipindi cha kampa kampa tena. Kamusoko kwenye ubora..Ngoma,Msuva nk...kwasasa hawajai sana uwanjani kama tulivyozoea.

Sasa hivi simba inajaza uwanja wa watu 60000 sababu ya kua bora tu na kupata matokeo mazuri sidhani kama Simba inahitaji support ya watu wengine ukiacha mashabiki wake.

Vilabu vijijenge vipate fanbase ukicheza vizuri utapata watu tu mashabiki wanataka matokeo mazuri tu wanahamia...ila siyo kusubiri watanzania wakushangilie sababu timu ni ya TZ...kila mtu ashabikie timu yake.
 
Back
Top Bottom