Simba nendeni Misri kukamilisha ratiba. Ukuta wa Yericko umegeuka kuwa ukuta wa biskuti, kila mechi bao

Majok majok

JF-Expert Member
Joined
Aug 3, 2023
Posts
783
Reaction score
2,057
Nilikuwa nawashangaa sana mashabiki wa hii timu walivyokuwa wanatamba sana mitaani wakijiapiza kumfunga Aly ahly goli za kutosha!

Lakini kwa wale wanaojitambua tulikuwa tunajua madhaifu ya mwakarobo na lilikuwa ni suala la muda tu kuzima tarumbeta zilizokuwa zinapigwa na vijana wa Rage, Baada ya dk 90 wimbo umebadilika umekuwa ule ule wa miaka yote waliyozoea kuuimba wa "TUMEKUFA KIUME"

Tokea nizaliwe sijawai kuliona ilo kombe la Kufa KIUME. Leo Mwakarobo Mganga wao alichowasaidia ni kupunguza idadi ya MAGOLI, kitendo Cha Aly Ahly kukosa zile nafasi 3 za wazi kwa macho ya kawaida unaweza ukadhani ni bahati mbaya lakini Ile ilikuwa ni kazi ya sangoma!

Ahly Ahly ilikuwa wambutue mtu goli 5 Leo but Mganga kaepusha aibu kubwa Leo. Na zile zilizokoswa wangekuwa kwao MISRI zilikuwa ni kamba kwa kuwa siku zote uchawi aupandi ndege ndio maana tulikuwa tunashuhudia sana zile goli tano tano kipindi kile!

Ndani ya mechi 8 ukuta wa yeriko umeruhusu kamba 9 kuchana nyavu zake, ndio maana tunasema safu Bora ya ulinzi itakupa makombe na safu Bora ya ushambuliaji itakupa magoli tu!

Mwakarobo najua mtakuja na mapovu kama yote lakini ayanibabaishi nawapa vidonge vyenu mkipenda mvimeze mkipenda mvitapike, timu yenu Ina shida kubwa kwenye eneo la kiungo mkabaji, uyo Ngoma mliyeenda sijui kumuiba uwanja wa ndege kwa mujibu wa msemaji wenu anaweza kutamba kwenye mechi za wakina JKT Tanzania na sio mechi kubwa za kimataifa, mechi za kimataifa utamuona Kama timu inamiliki mpira lakini Kama timu inapekekewa moto ni sawa na yale mapazia ya buku buku yanoyouzwa mnadani!

Sasa keshokutwa mnakwenda Misri kukamilisha ratiba yenu kwakuwa kule akuna kuvunja Nazi Wala kuchoma uwanja uwezo wenu halisi unakwenda kuonekana mjipange na Ligi kuu na makundi ya klabu bingwa!

MAPOVU YA OMO NA KLEESOFT YANARUHUSIWA KWA WAFUASI WA MBUMBUMBU!
 
Ila kuna baadhi ya watanzania ni wapumbavu sana, mlitegemea Simba kupigwa nyingi, ila mmeona mpira ilivyotembea.

Siwadai chochote Simba tutazidi kuimarika.

Uzuri Al Ahly mnao kundi moja tutaona[emoji1374][emoji1374][emoji1374][emoji123][emoji881][emoji881]
 
kitendo Cha Aly Ahly kukosa zile nafasi 3 za wazi kwa macho ya kawaida unaweza ukadhani ni bahati mbaya lakini Ile ilikuwa ni kazi ya sangoma!!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unafkiri hata ukiwadai wana uwezo wa kukulipa sasa!

Makolo shukuruni kwa kushiriki.
 
Utawadai na cha kukulipa watakitoa wapi Sasa, mpira wa kisasa unatakiwa uwekeze kwenye benchi Bora la ufundi na wachezaji Bora watakaokupa matokeo popote iwe nyumbani ama ugenini, na sio kuwekeza kwenye mambo ya nje ya uwanja ndio maana mkitoka nje mnakuwa na wakati ngumu sana kwakuwa matunguri yanakuwa yamebaki dar es salaam!
 
Uliyaona hayo matunguri? Imani potofu zimejaa kwenye mafuvu yenu, kipi cha ajabu? Yaani wao kukosa goli wamelogwa?

Ujinga mtupu, football imechezwa vizuri kwa ufundi.
 
Hujui Mpira..mbona hao Ahly wameruhusu magoli..hakuna timu isiyofungwa
 
Mechi bado haijaisha, Simba kutandikwa tano pale Cairo halitakua jambo jipya.
Mbaya zaidi mwekezaji wenu mlipo pata goli akawa anajipiga kifuani mbele ya Rais wa Ahly, yaani alikua ana mtambia.
Sasa kile kitendo kinaweza kikasababisha mtandikwe ata zaidi ya tano pale Cairo.

Sent from my SM-A032F using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…