Simba nyinyi ni Wetu kelele za nini?

ibanezafrica

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2014
Posts
7,261
Reaction score
6,553
Jana yanga tumepoteza pointi tatu muhimu katika mechi dhidi ya Rivers united ya Nigeria Simba wametuzomea sana kana kwamba hawajui hali yetu.

kwa sasa tujuavyo Simba kwetu sisi ni mke wetu..na mara zote mke huwa anajua raha na karaha zote anazopitia mume wake
Sasa ajabu simba wanajitoa akili kujitia ati hawajui magumu tunayopitia ikumbukwe ligi msimu huu zilichelewa kuisha Yanga tumesajiri pamoja na kuuza wachezaji.

Muda wa maandalizi na kuzoeana wachezaji pamoja na benchi la ufundi umekua finyu mno...mbali na hayo wachezaji wetu watatu maahiri na muhimu kwetu wamezuiwa kushiriki mchezo huo wa jana hii imepelekea yanga kushindwa pata matokeo mazuri.hizo ndiyo sababu kubwa na tatizo lililopo jangwani lakini bado tuna imani kubwa na timu pamoja na mwalimu.

Simba acheni kuongea sana wakati mnajua fika hali yetu lakini tulieni tunakutana katika ligi na huko tuendapo mbona mtaomba poo!
 
We kweli ni Utopolo ,hata hujui unachoandika , unasema jana mmepoteza point 3 kwani mpo kwenye makundi? Huu ni mtoano hakuna point .

Endeleeni kujipanga kwa ajili ya kuifunga Simba na siku ya mwananchi ila siyo makombe
 
Your browser is not able to display this video.
 
... Yanga tumesajiri pamoja na kuuza wachezaji...muda wa maandalizi na kuzoeana wachezaji pamoja na benchi la ufundi umekua finyu mno...
Hata mwaka juzi na mwaka jana, wachezaji wa Yanga walishindwa kuzoeana hadi misimu inaisha. Msimu huu itakuwa wimbo huo huo pia!
 
MTOANO HAUNA POINTS TATU ZINAANZIA MAKUNDI AMBAYO HAMNA UWEZO Wa KUFUKA MJIPANGE KUPATA TOP FOUR LIGI YA BONGO MSUBIRI SIMBA IHANGAIKE KUFIKA ROBO FAINALI HUKU MKIIPIGA VITA NA KWENDA KUPOKEA WAGENI AIRPORT
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…