Simba Panthera - Fact File

adden

JF-Expert Member
Joined
Dec 27, 2015
Posts
7,033
Reaction score
15,638
Simba ndiyo mnyama mkubwa kuliko wote katika jamii ya paka. Simba hupatikana Afrika na Asia, idadi yao ikitizamiwa kufikia 23000(elfu 23), huku Tanzania ikiongoza kwa kuwa na idadi ya zaidi kuliko nchi zote. Simba wako katika hatua ya kutoweka (vulnurable).

Ndiye mnyama pekee jamii ya paka anaeishi kifamilia, hii inapelekea kuwa ndiye mnyama anayeweza kufanikiwa zaidi kulingana na umoja wao. Kufanikiwa huku ni pamoja na mawindo yao au ulinzi kwa familia kiujumla.

Simba dume wakifika miaka 3 hufukuzwa na baba zake ili wakajitafutie maisha yao, sababu nyingine wasipate muda wa kutoka na dada zao au shangazi zao, pia wasije kupindua nyumba na kurithi utajiri wa familia.

Simba akishafukuzwa kwenye familia huunda genge lao (coalition), iwe ni ndugu au rafiki atakayekutana naye huko porini. Baada ya hapo huwinda pamoja na wakikuta familia ina simba dume dhaifu basi humpiga au kumuua kisha kuirithi ile familia, na wakati mwingine wakikosa hurudi alipotoka kwa baba yake kumfanyia uharamia huo!

Wakisharithi wanaanza kufagia kizazi cha dume aliepita, kama mtoto ana chini ya mwaka 1 huua. Sababu hii hufanya jike aache kunyonyesha na kuingia kwenye kipindi cha hedhi (heat), sababu nyingine ya kuua ni kutaka kuwe na kizazi chake tu, siyo watoto wa baba mwingine.

Kufanya mapenzi kwa binadam au jamii ya nyani kunaweza kuwa ni starehe sana. Lakini kwa simba ni mateso makubwa sana. Baada ya jike kuingia kipindi cha kupata mimba, basi wale madume au dume hujitenga na familia.

Hufanya mapenzi kila baada dakika 20 kwa siku 5, ambako siku ya 3 dume huwa amechoka sana hivyo kumuachia dume mwingine amalizie siku zilobaki. Kama yuko mwenyewe itabidi apambane siku 5 ziishe. Simba jike mayai yake huchavushwa taratibu sana (low rate of fertility), hivyo kila muda wa tendo dume hutumia uume wake wenye miiba (barbed penis) ili kumpa hamu.

Sababu ya kupiga mtungo jike mmoja madume wawili ina sababu zake, hasa ili dume wote wajue mtoto atakayeezaliwa ni wao (confuse partenity). Simba hubeba mimba kwa muda wa miezi mitatu na nusu (siku 100).

Mtoto huzaliwa akiwa haoni na humtegemea mama kwa kila kitu (atricial), tofauti na nyumbu au nyati hubeba mimba zaidi ya miezi 8 na mtoto akizaliwa huweza kuona na kutembea na mama yake kwa wakati huo (precocial), sababu mtoto hukua tumboni kwa muda mrefu tofauti na paka.
Mtoto simba akifikisha mwaka 1(mmoja)mamaake anakuwa amefanya mapenz mara elfu 3.

Turudi kwa simba, baada ya wiki 4 kutoka mafichoni vitoto vya simba hupelekwa kutambulishwa kwenye familia. Ikiwa kuna simba jike mwingine ana watoto wakubwa (miezi 3 au 4), basi yule simba mzazi huacha ipite wiki 7 ndiyo hupeleka kutambulisha wale watoto.

Sababu kubwa ni kuwa simba watoto wote hunyonya kwa mama yoyote (cross milking), hii ni lazima kwa simba mtoto kunyonya kwa mama tofauti, hii huchangia ukuaji haraka.

Simba jike ndiye mwindaji sababu ni mwepesi na anaweza kujificha kirahisi. Jike wakishapata windo hawali hadi dume aje kuanza kula. Muda mwingine dume anaweza kumaliza msosi wote mama na watoto wakakosa na jike hawezi kufanya chochote sababu dume ana nguvu na ndiye mlinzi wa familia.

Ulimi wa simba ni kama msasa, kwa kulamba tuu huweza kutenganisha mfupa na nyama. Dume hula hadi kilo 8 za nyama.

Jike huishi maisha marefu kuliko dume, ambapo dume hazidi miaka 15 hufariki. Nywele za simba dume zikiwa nyeusi ndiyo anakuwa na testorone nyingi (handsome) na nywele humsaidia simba dume asiumie shingoni wakati wa mapigano.

Simba hunywa maji lakini pia kiu yake hupoozwa na damu ya windo wakati wanakula (blood meat). Dume huwa na uzito wa kg 180 huku jike akiwa na 130. Simba hukimbia (top speed) 60kph.

Ni hayo machache, kama yupo anaweza kuongezea, karibuni.
 
TEMBO-fact file

Ndie mnyama mkubwa kuliko wote wa nchi kavu.
Tembo hupatikana africa kwa wingi na asia.

Tembo wa africa ni wakubwa kuliko wa asia.tembo wa africa hufikia hadi tani 7(kg7000).hula majani matunda na magamba ya miti.kwa siku tembo mmoja hula kilo300 za majani na lita200 za maji.
Usagaji chakula tumboni kwa tembo ni mdogo sana yaani 40% ya chakula chote hula kwa siku ndio husagwa(digestion).hujisaidia kilo150 ya kinyesi kwa siku.kinyesi chake sababu hakisagwi vizuri basi huwa ni chakula kizuri kwa wanyama wengine kama ndege na nyani.vile vile kinyesi cha tembo kinaaminika katika usambazaji wa mbegu na kuotesha miti huko mbugani.ikimaanisha bila tembo basi mbuga zote ingekuwa ni majangwa.ukiwa mbugani hutakiwa kukanyaga kinyesi cha tembo kwasababu ni chakula cha wanyama wengine ikiwemo wadudu kama biringita mavi(dung bettle).dung bettle ndie mdudu anaeweza kusukuma kinyesi kikubwa mara elf8 ya uzito wake.yaani kama binadamu uisukume ndege ya airbus!..

Meno ya tembo(tusks)hutumika kama mkono wa kuchimbia mashimo ili kupata maji.kuangusha miti ili kufikia matunda yaliyopo juu.pia kwaajili ya kuugemezea mkonga wake(trunk).Trunk(mkonga)hutumika kama mkono na vidole kwaajili ya kula chakula kuvuta pumzi.kunywea maji na kuogea.maskio makubwa ya tembo hutumika kama feni kipindi cha joto kali.
Shingoni kwa tembo kuna ngozi laini iliyopitisha mishipa mingi ya damu(cappilaries).ikiwa joto sana basi tembo automatically husukuma lita 12 ya damu kila dakika hapo shingoni kisha hupepea maskio yake damu hupoa na kuirudisha mwilini.kipindi cha baridi kali tembo hubana maskia yake ili kutunza joto lisitoke.skio moja la tembo lina mita2 na uzito wa kilo 20.humfanya tembo kuweza kusikia mapigo yako ya moyo ukiwa mita 5.

Tembo hubeba mimba kwa miezi 22.mtoto huzaliwa na kilo60 au 70.
Kipindi cha uzazi ndugu wa tembo humletea chakula mzazi ikiwemo miti yenye matunda na majani.mtoto tembo hunyonya mkonga wake kama mtoto ananyonya kidole.inaaminika duniani na mbinguni hakuna mnyama anaempenda mtoto wake kama tembo.tembo humfundisha mtoto wake tabia njema(good manner).kuanzia adabu ya kula na heshima kwa wakubwa!.

Tembo dume hubalehe akifika miaka 14.
Hujitenga na wazazi na huishi katika bachelor group.akifika miaka 40 ndio hutafuta mke na kuanzisha familia
Tembo jike hubalehe mapema zaidi na huanza kupandwa muda huo huo.
Wakati jike anabalehe anakuwa na tani 1.5 na dume anakuwa amefikia (full matured) na uzito wa tani6 hadi 7.hivyo jike hupata shughuli maana tani 7 kuja juu sio mchezo.pia tembo uume wake mkubwa sana una kilo15.akishampanda jike hummwagia manii lita3.

Tembo huishi hadi miaka 60.
Hufa kutokana na meno kuisha hivyo kushindwa kula.
 
Lion ni vulnerable kwenye iucn criteria 3.1 Acha urongo mkuu
 
Kati ya simba na chui milia, yupi mkubwa zaidi?
 
Fisi- fact file

Fisi ni mnyama mkubwa wa pili katika kundi la wala nyama(carnivores).hufikia kg80 kwa jike na 50kg dume
Fisi pia ni aina ya wanyama wanaoishi kifamilia.hafungamani sana kitabia na jamii ya mbwa bali kidogo anaweza kuingiliana na jamii ya paka(FELIDAE).

Fisi jike ndio kiongozi katika ukoo!
Fisi jike ana umbile kubwa kuliko dume.vilevile jike ana homoni nyingi za kiume kuliko dume(testorone).
Fisi jike huzaa watoto 2 au 3 na hubeba mimba kwa miezi 4.kama jike ndie mkuu wa ukoo basi watoto wake wa kike ndio watarithi ukuu.
Fisi jike ana uume(7 inch) na makende!
Lakini kiuhalisia ile sio uume ni (kinembe)na yale makende ni mashavu ya uke(labia majora).fisi husalimia kwa kutumia sehemu zao za siri!
Jike hutumia kinembe chake kwa kutolea haja ndogo,kufanyia mapenzi na kuzalia...!
Jike hupata wakati mgumu sana kujifungua hata kupelekea kifo sababu njia anatoka mtoto ni ndogo sana.
Mtoto wa fisi huzaliwa tayari anaona na vile vile meno yametoka na anaweza kula nyama.


Fisi ni wawindaji wazuri sana.
Fisi wakipata windo au mzoga hula wakishiba hula tena ili kubeba akiba ya chakula kwa ajili ya watoto wao.wakifika kwa watoto hutapika ile akiba kisha watoto hula.fisi ndie bwana afya porini pasipo fisi basi magonjwa yangetapakaa na viumbe wengine wangetoweka.
Wana nyongo kali inayoweza kuyeyusha mifupa,kucha,pembe hata ngozi.muda mwingi fisi akitoka kula huwenda kulaza tumbo lake kwenye maji ili kupooza injini ya tumbo..
 
Basi simba sio mnyama mkubwa zaidi kwenye kundi la wanyama jamii ya paka.
Kuna simba unaweza kukuta ni mkubwa na mzito kuliko tiger.hii inategemea wapi na wapi.maana rekodi inaonyesha wamepishana kg20 au 10kg.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…