Lucchese DeCavalcante
JF-Expert Member
- Jan 10, 2009
- 5,471
- 752
KLABU ya Simba imeanza kupukutishwa fedha zake za mapato baada ya kukatwa Sh3 milioni katika pambano lao na Azam kwa ajili ya kukusanya fedha za kumlipa winga wake, Haruna Chanongo, anayecheza kwa mkopo Stand United Mwanaspoti linaweza kuthibitisha.
Chanongo aliiburuza Simba baada ya kuona inamyeyusha kuhusu mshahara wake wakati Stand ikitekeleza kwa asilimia zote makubaliano ya kulipa sehemu iliyobaki ya mshahara wake.
Mbali na fedha inazodaiwa na Chanongo, Simba pia imetakiwa kumlipa mshambuliaji wake wa zamani, Amissi Tambwe kiasi cha Dola za Kimarekani 7,000, wakitakiwa kuanza kulipa Dola 5,000 kisha kumalizia Dola 2,000 kabla ya Mei 10 kutokana na kuvunja mkataba na kukiuka makubaliano ya kulipana fedha hizo kabla ya Desemba 17 mwaka jana.
Simba ilimtema Tambwe Desemba 14 na mchezaji huyo kukimbilia Yanga na kuahidiwa kupewa fedha zake mapema, lakini ikawa inapiga danadana na hivyo mchezaji huyo akakimbilia TFF ambako Kamati ya Sheria na Hadhi ya Wachezaji ya TFF ilisikiliza kesi hiyo na nyingine na kutoa maamuzi hayo.
Ni wazi uamuzi wa kuanza kukata makato ya Simba unaiacha klabu hiyo katika wakati mgumu kwani ni fedha ambazo zingeweza kufanya kazi nyingine kama madeni hayo ya wachezaji hao yangekuwa yamelipwa kwa mujibu wa wakati.
Chanzo: MwanaSpoti