Simba sasa waanza kutemeshwa noti

Lucchese DeCavalcante

JF-Expert Member
Joined
Jan 10, 2009
Posts
5,471
Reaction score
752
KLABU ya Simba imeanza kupukutishwa fedha zake za mapato baada ya kukatwa Sh3 milioni katika pambano lao na Azam kwa ajili ya kukusanya fedha za kumlipa winga wake, Haruna Chanongo, anayecheza kwa mkopo Stand United Mwanaspoti linaweza kuthibitisha.

Chanongo aliiburuza Simba baada ya kuona inamyeyusha kuhusu mshahara wake wakati Stand ikitekeleza kwa asilimia zote makubaliano ya kulipa sehemu iliyobaki ya mshahara wake.

Mbali na fedha inazodaiwa na Chanongo, Simba pia imetakiwa kumlipa mshambuliaji wake wa zamani, Amissi Tambwe kiasi cha Dola za Kimarekani 7,000, wakitakiwa kuanza kulipa Dola 5,000 kisha kumalizia Dola 2,000 kabla ya Mei 10 kutokana na kuvunja mkataba na kukiuka makubaliano ya kulipana fedha hizo kabla ya Desemba 17 mwaka jana.

Simba ilimtema Tambwe Desemba 14 na mchezaji huyo kukimbilia Yanga na kuahidiwa kupewa fedha zake mapema, lakini ikawa inapiga danadana na hivyo mchezaji huyo akakimbilia TFF ambako Kamati ya Sheria na Hadhi ya Wachezaji ya TFF ilisikiliza kesi hiyo na nyingine na kutoa maamuzi hayo.

Ni wazi uamuzi wa kuanza kukata makato ya Simba unaiacha klabu hiyo katika wakati mgumu kwani ni fedha ambazo zingeweza kufanya kazi nyingine kama madeni hayo ya wachezaji hao yangekuwa yamelipwa kwa mujibu wa wakati.

Chanzo: MwanaSpoti
 
Sasa kama wanashindwa kumlipa Chanongo kweli msuva wanaemtaka watamuweza kweli!!!!
Tena nasikia hata ndoa yao na TBL inavunjika Jumamosi ya tar. 09/05/2015 baada ya timu ya simba kushindwa kushiriki mashindano ya kimataifa kwa misimu mitatu mfululizo.......
 
Hilo ni litimu la hovyo kupata kutokea duniani yenyewe yalisema hivi eti "ubingwa si malengo yetu kama klabu ila lengo letu kuu ni kuifunga Yanga basi hapo tutakuwa tumemaliza ligi " kwa hiyo hata mambo ya kifedha haikuwa kwenye malengo kama klabu, wanasahau kuwa wadhamini wanafuata mafanikio ya klabu sio kuuza sura
 

Mimi hupenda sana kusikia habari mbaya za mikia, asante sana Mkuu mkolaj kwa kunifurahisha siku ya leo.
 
Last edited by a moderator:
Bwanawao hanshope anakiritimuiko halimbaya hanahelakama Manji ooh tff waangalieupya Mbonaunacheka


Haahaaaq wamekula dili zausajili
NIWAJULISHE tu Ndiomaana kukawanamgawanyiko palejuu kunawachezajj wakiletwa nakiongoz anakata samuammaunntii sasa HILI presidaa wakamgeuka mnajua alieletawachezaji pale hapo. ikawashidaaa naakunakuelewana maana jamaa alisajili akalachajuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…