Simba Sc 1-0 RS Berkane | CAF Confederation Cup | Benjamin Mkapa Stadium

Simba Sc 1-0 RS Berkane | CAF Confederation Cup | Benjamin Mkapa Stadium

Greatest Of All Time

JF-Expert Member
Joined
Jan 1, 2017
Posts
23,620
Reaction score
52,790
Leo ni sikukuu kwa wapenda kandanda nchini Tanzania.

Mnyama Mkubwa mwituni, Simba Sc atashuka katika dimba la Benjamin Mkapa kucheza dhidibya RS Berkane ya Morocco majira ya saa 10:00 jioni kwa saa za Afrika Mashariki.

Simba itaingia dimbani huku ikiwakaribisha nyota wake waliotoka majeruhi kama Chris Mugalu, Kibu Denis, Jonas Mkude, Tadeo Lwanga, Bwalya huku ikiwakosa Hassan Dilunga na Chama (ambaye sheria zinambana)

Simba itahitaji ushindi wa hali kwa mali ili kujiwekq katika nafasi nzuri ya kufuzu kwenda robo fainali ya michuano hiyo.

RS Berkane wakiwa ugenini wamekuwa na tabia ya kuruhusu magoli hivyo Simba ikitulia vizuri leo wanaweza wakavuna alama 3 muhimu.

Mechi ni saa 10:00 kupitia Utv ya Azam Tv.

Mijadala, updates na yote kuhusu mechi hii utapata dondoo kupitia uzi huu...karibuni sana

Simba nguvu moja!!

=====

44' ⚽Sakho anaitanguliza Simba kwa goli murua, Simba 1-0 Berkane

45' Dakika nne zimeongezwa kuhitimisha kipindi cha kwanza, Simba SC VS RS Berkane

90+4' Filimbi inapulizwa kuashiria mwisho wa mchezo na Simba inashika usukani wa kundi D ikiwa na alama 7.
 
Yanga wajue kabisa kucheza ndondo na wasomali Kisha kuiita mechi ya kimataifa kutawaponza RS Berkane.
Naukizingatia yanga ipo kundi gumu sana, we ucheze na Somalia, Ukraine na urusi....Kuna kupona hapo.
Kundi la yanga
Yanga
Somalia
Ukraine
Russia
 
Leo sijavaa kabisa jezi ya chama langu. Hii ni kutokana na uchunguzi binafsi niliojifanyia.

Yaani siku nikiwa na mzuka sana wa mechi na matokeo yangu kwapani basi tunalazwa na viatu lakini leo nimetulia kabisa moyoni na leo naona kabisa Rs Berkane wataponzwa na damu ya kisinda maana tutajipigia zileee nne kwa moya km kawaida yetu.

Ukibisha sema su na ukisema tunakuongezea kipigo na km hujibu ukweli unaujua wa kutuogopa.
 
Back
Top Bottom