Simba SC Haijaandaliwa Kimfumo wa KNOCK-OUT-

Megalodon

JF-Expert Member
Joined
Apr 9, 2021
Posts
3,534
Reaction score
7,866
Pamoja na yote tukubali kuwa SSC haitoweza kucheza nusu fainali.

Hii ni kwasababu timu hiyo haijawahi kuandaliwa kwa mfumo wa knock out.

Ni kikosi kimoja tu mimi nakiita kikosi cha dhahabu chini ya Gomez ndiyo kilikuwa na uwezo wa kukaza ugenini, kushinda au kutoa suluhu. Mikisoni -Morisson -Chama, Bwalya -etc etc

Kikosi cha sasa SSC ni kile cha kula goli 5 ugenini , hata 10 . Asec angekuwa Serious kidogo angemla simba hata goli 10.

Ugenini simba inakuwa WEAK sana na inafungika kirahisi sana, huku Pablo akikosa uwezo wa kucheza away games.

Nasema kwamba SSC anaweza kushinda hata goli tatu pale LUPASO, kwa Hayati BWM , lakini akienda away hizo goli zinarudi kipindi cha kwanza tu.

Ndugu zangu tujiandae ki fikra ili kupunguza machungu, mpira sio matangazo au mihemko ya mashabiki, mpira ni investment na kuwa nawachezaji wenye uwezo wa kusababisha popote.

Naiombea SSC kheri lakini ukweli ni kwamba mpira sio dua, mpira ni ushindani na kuwa nawachezaji wa maana.

Mazingira ya SSC kutolewa ni asilimia 90 .

Sina imani na safu butu ya ushambuliaji na beki yenye kupwaya.

Time will tell
 
Barcelona na Bayern wana maoni gani juu ya hili?
 
Sawa tumekusikia. Anza safari kuelekea airport kupokea wageni na kuwaandalia maji ya kuoga..Ndiyo Kazi mliobakiza pamoja na umbeya.
 
Hivi ng'ombe fc iliyo kundi Moja na wahanga wa vita vya somalia Jumapili itakuwa inamenyana na timu gani kwenye kundi lao? Au na wao walishafuzu hatua ya robofainali?
Achana na ng'ombe fc, msimu huu TPL ishakuwa yao, wana timu ambayo wakionheza nguvu kidogo tu wanaweza msimu ujao wakafanya vizuri michuano ya afrika.

Tudeal na mambo yetu sisi, TPL tunaikosa, na uwezekano wa kuvuka hapo ni mdogo kiukweli, tuweke nguvu tutoboe hapa, tuchukue na shirikisho hii itakuwa walau inatupoza machungu.
 
Sawa tumekusikia. Anza safari kuelekea airport kupokea wageni na kuwaandalia maji ya kuoga..Ndiyo Kazi mliobakiza pamoja na umbeya.

Je nimeongea uongo ? Tusubir, ninahakika kwa asilimia 90 huu ndio mwisho. Hamna kikosi cha ku play away games
 
Mlianzaga kupokea wageni kwa mkapa mkitegemea tutafungwa ,baada ya kuona Simba haipotezi game mkaacha taratibu na kuona aibu,Sasa hivi mnategemea Simba kupoteza ugenini bila kuwaza je nyumbani akishinda mengi je?

Poleni sana

Naomba urudi baada ya wiki 2
 
Hivi ng'ombe fc iliyo kundi Moja na wahanga wa vita vya somalia Jumapili itakuwa inamenyana na timu gani kwenye kundi lao? Au na wao walishafuzu hatua ya robofainali?

Topic ni ya Simba
 

Yanga bingwa.SSC anasuasua sana
 
Kuna tatizo la hasira hapa.Mtu anaandika huku kakabwa na hasira kooni.Kisa?Simba kucheza robo fainali.[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Urudi hapa ndani ya wiki 2 ndio utajua kutofautisha ukweli mchungu na mawazo finyu. Hamna uwezo wa kufanya knock out , unawapampu mashabiki na kuwaaminisha uongo wakati mnajua kutoboa ni Haiwezekani
 
Urudi hapa ndani ya wiki 2 ndio utajua kutofautisha ukweli mchungu na mawazo finyu. Hamna uwezo wa kufanya knock out , unawapampu mashabiki na kuwaaminisha uongo wakati mnajua kutoboa ni Haiwezekani
Kwa hiyo unakesha ukiomba mawazo yako yatimie?Mna shida sana.πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…