Simba SC, hii sasa sifa...

sembo

JF-Expert Member
Joined
May 25, 2011
Posts
4,350
Reaction score
3,451
Jana jioni, Simba SC iliingia uwanjani kujipima nguvu tena. Ilikua ni zamu ya timu ya Jang'ombe Boys toka Visiwani humo ambapo, walitandikwa goli 3-0.. Ni yule yule mchezaji aliye kwenye kiwango bora kwa sasa, Elias Maguli ndo alikua wa kwanza kuandika goli dk. ya 14.. Dk ya 17, Michael Mgimwa aongeza la pili, na aliyefunga kalamu ni Samir Omar katika Dk. ya 81.
Baadhi ya picha za gemu la jana:

View attachment 273437

Mabeki toka Zenji bhana, wanazani ili kuwazuia washambuliaji wa Simba SC unatakiwa ucheze kama Rugby.. Hapa Maguli aligeuka kidogo tu, beki akabaki anaduwaa tu.. Then jamaa akatupia kambani.

View attachment 273440

Hapa wachezaji, wakifurahia moja ya goli lililofungwa jana.

Hii ilikuwa ni mechi ya NNE kujipima ubavu, tangu Dylan Kerr.. Hebu cheki baadhi ya takwimu hapa chini.

Idadi ya Mechi... 4:

Goli za kufunga... 11:

Goli za kufungwa... 1:

Ukiangalia hizo data hapo juu.. tunagundua kua sasa defence yetu imekwiva vya kutosha, ile Great Wall of China imeshakamilika.. Kiungo imeimarika sana, ndo maana kina Maguli wanatupia kila wanavyotaka.. Sasa sipati picha Mwinyi Kazimoto a.k.a Ball Dancer, nae akiwa ndani, si kuna baadhi ya timu zitakua zinaogopa kurudi 2nd half?!

BONUS:
Kiungo mkabaji bora kabisa kuwahi kushudiwa nchini Zimbabwe yupo na timu ya Simba SC Unguja, akiangaliwa kwa umakini na Kocha mwenye Leseni A ya UEFA, ili asajiliwe.. Jina lake ni Justice Majbvi.. Naamini atampush sana Jonas Mkude, maana huyu dogo alikua hana mpinzani.
Hebu cheki mavitu yake hapa akiwa uwanjani.. Huyu jamaa ni mtu wa kazi asikwambie mtu.





Pia kazoea kubeba makombe.. Ambayo atakutana nayo msimu wa 2015/2016.





Kama mambo yataenda sawa, leo itakua zamu ya KMKM kukutana na dhahama la Simba SC.. Na hii inaweza ikawa mechi ya mwisho ya kujipima.

".. na Simba Day ifike mapema" - Sembo
 
Mavugo yupo

Mkuu, kuhusu Mavugo.. Vital'o wameongeza dau maradufu tofauti na makubaliano ya awali.. Ila kuna binadamu anaitwa Danny Lyanga toka Daring Motema Pemba a.k.a DC Motema Pembe ameshatua kuziba pengo la Mavugo.
Danny Lyanga ni nani?

- Kazaliwa 28/07/1991 (miaka 24) jijini Arusha

-Baada ya kucheza soka kwa kiwango cha juu kabisa mitaani, msimu wa 2010/2011 akiwa na miaka 19 tu, alitua timu ya Arusha FC na kuingia moja kwa moja 1st eleven, ambapo rekodi yake ya kutupia magoli ni ile ile kama ya Mavugo.. Mechi moja, Goli moja au zaidi

-Kutokana na kuonesha kiwango bora msimu uliofuata alitua Coastal Union, ambapo alicheza misimu miwili. Msimu wake wa mwisho alitupia goli 7, na goli la mwisho kufunga lilikua katika uwanja wa Mkwakwani dhidi ya timu yako (Azam FC) na gemu iliisha 1-1.. Na siku hiyo Ndala wakatangaza ubingwa wakiwa na mechi mbili mkononi.

-Msimu ukiofuata, alijiunga DC Motema Pembe.. na hii ni baada ya kuzipiga chini Simba, Ndala na Azam.

- Msimu uliopita, mkataba wake umeisha.. Hivyo anatua Simba SC akiwa huru.

KARIBU SANA SIMBA SC.. Mshambuliaji hatari, Danny Lyanga.
 
hivi simba walishatolewa sports extra ndondo cup?
 
Mkuu hivi wewe ndo mhariri wa kijarida cha kufungia maandazi cha ngurumo za mikia nini????
 
Mechi na timu za mchangani nazo zakujisifia?
 
hivi simba walishatolewa sports extra ndondo cup?

Mkuu, kikosi chetu kilkua bado hakijaiva.. Sasa kimeshanoga, tunasubiri kwa hamu Mtani Jembe Bonanza Cup.
 
Sembo kwema ndg yangu?kiukweli ushabiki kama wako au unazi ni kitu cha kujivunia sana sababu mahaba ya kupenda vya kwetu yameisha.Mimi ni kandambili, ndala,kualalumpa(kwala)gongo wazi daima mbele ila nakupongeza kupenda vya kwetu.
 
Sembo kwema ndg yangu?kiukweli ushabiki kama wako au unazi ni kitu cha kujivunia sana sababu mahaba ya kupenda vya kwetu yameisha.Mimi ni kandambili, ndala,kualalumpa(kwala)gongo wazi daima mbele ila nakupongeza kupenda vya kwetu.

Mkuu pamoja sana.
 
Mkuu, kikosi chetu kilkua bado hakijaiva.. Sasa kimeshanoga, tunasubiri kwa hamu Mtani Jembe Bonanza Cup.
mlivyompoteza okwi nikajua mmepoteana. mlivyompata mavugo nikaona mnarudi. tena mnampoteza!!
 
Mkuu hivi wewe ndo mhariri wa kijarida cha kufungia maandazi cha ngurumo za mikia nini????

Hapana Mkuu, mimi ni mwanachama wa kawaida, mwenye mahaba ya dhati na Simba SC.
 
mlivyompoteza okwi nikajua mmepoteana. mlivyompata mavugo nikaona mnarudi. tena mnampoteza!!

Mkuu.. kuna fitina zilipigwa baada ya kusikia kuwa Mavugo kashachota kati ya dola 10000 na 20000, huku Simba ikiwa bado kuwakabidhi Vital'o mkwanja wao.. Simba walipopeleka fungu vital'o, jamaa wakageuka.
Ila hakuna noma, ndani hizi siku mbili tatu kabla dirisha la usajili halijafungwa, tegemea kua wakwanza kusoma usajili mpya katika http://simbasports.co.tz/ .. na naamini utatikisa nchi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…