GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 60,660
- 121,325
Hivi ni kwanini Viongozi wa Simba SC ( Timu yangu Kipenzi kabisa ) huwa hamna utaratibu wa kupitia Mtandao huu wa JamiiForums ili muwe mnatusoma akina GENTAMYCINE na ' Wadau ' wengine wa mpira ili muwe ' mnaokota ' machache na mnayawasilisha katika Benchi la Ufundi linaloongozwa na Kocha Pierre Lechantre?
Namshukuru Mwenyezi Mungu tu kwamba jana tumeweza ' Kujitutumua ' na kutoka suluhu / sare na Wapinzani wetu Al Masry kutoka nchini Misri katika michuano ya CAF CC ambayo tunashiriki ila leo nina ' dukuduku ' langu kubwa ambalo nataka kulitoa hapa kwani nimegundua kila mara Simba SC tunaharibu Kimataifa na hata nchini hapa kwa makosa ya Kiufundi kabisa ambayo nadhani Timu kubwa kama Simba SC ingeweza kuyajua mapema.
SAIKOLOJIA
Natambua na pia kupongeza sana juhudi za Mwanasaikolojia ' Nguli ' nchini Chris Mauki kuweza kuwapa ' ushauri ' wa Kisaikolojia Wachezaji wa Simba SC kitu ambacho kimeweza kusaidia maeneno fulani ila nilidhani Benchi la Ufundi lingefanya zaidi ya ' Mtaalam ' Mauki.
Inahitaji akili ndogo tu kujua kwamba siku zote Saikolojia na Waarabu tena ' Wamisri ' huwa wakija ' Ugenini ' hupenda mno kucheza kwa taratibu huku wakivizia ili kuwapozesheni na nyie yote hii ikiwa ni katika hali ya ' Kujilinda ' kutokufungwa na hii mbinu yao huwa inawasaidia sana.
Mara nyingi sana jana niliwaona Wachezaji wa Simba SC wakicheza kwa taratibu, kutokuwa wachangamfu hasa katika kuanzisha mpira na badala yake nao wakawa wanawaiga Wamisri hali ambayo iliweza kuifanya Simba SC kuchelewa kupeleka mashambulizi mbele na hata kutucheleweshea ushindi.
UPANGAJI TIMU
Hii ni mara ya pili leo naandika humu JF masikitiko yangu makubwa hasa juu ya Upangaji wa Kikosi cha Simba SC na nakumbuka hata katika makundi mengine ya Mitandao ambayo nipo hadi katika ' Vijiwe ' vyetu huwa nalilalamikia na kuna waliokuwa wakiona nimepotoka ila nashukuru Mungu wengi wao jana baada ya mechi walianza kunielewa.
Wana Simba SC hata msemeje au mfanye nini Safu yetu ya Ulinzi haiwezi Kukamilika kwa 100% kama Beki ambaye kwa sasa bado sijaona anayemfikia kwa huu ukanda wetu Mganda Juuko Murshid na najiuliza hadi leo ni kwanini sasa hivi hapati nafasi Kikosini wakati Timu ya Taifa ya Uganda ambayo imetuzidi Tanzania mbali mno kwa Viwango viwe vya CAF na FIFA ndiyo Beki wao tegemeo kabisa.
Simba hivi ni kweli kabisa inaingia akilini leo hii unamuanzisha Yusuph Mlipili kucheza nafasi ya Ulinzi na unamuacha Juuko Murshid benchi? Sisemi kwamba Yusuph Mlipili hafai au hajui la hasha tena hakuna Beki ambaye kama Simba SC tutamlea vyema atakuja kutusaidia baadae Kikosini kama Yusuph Mlipili ila tusidanganyane bado hana ' experience ' na mechi kubwa na kama mtakuwa makini jana aliweza kufanya makosa makubwa sana kule nyuma na kuigharimu Timu mara kwa mara hadi kumfanya James Kotei kupotea huku Jonas Mkude na Erasto Nyoni wakijitahidi kumfuatia makosa ( Yusuph Mlipili )
Simba SC acheni ' uswahili ' wenu na msidhani Sisi akina GENTAMYCINE labda hatujacheza mpira au hatujui mpira tena wengine leo tukisema turudishe nyuma miaka na muone jinsi tulivyokuwa tukicheza ' Soka ' labda mngetusajili kwa ' Mipesa ' mingi sana sema tu ' majukumu ' mengine yalitutinga na kuamua kuachana na kucheza mpira. Tunaomba Beki Juuko Murshid arudishwe katika ' First Eleven ' ya Timu ili kuifanya ' defensive line ' ya Timu kuwa ' solid ' na ya uhakika zaidi kuliko hii ya sasa iliyo chini ya Yusuph Mlipili ambayo mara nyingi huwa inatufanya Sisi ' mashabiki ' huku Jukwaani kuwa na wasiwasi na uwoga.
MUDA WA MCHEZO NA NAFASI YA KOCHA KWA TIMU
Nilimwelewa sana na mno Kocha wetu Pierre Lenchatre hasa pale aliposema kuwa amesikitishwa na Uongozi wa Simba SC kuamua kuupeleka huo mchezo Saa 12 jioni badala ya kucheza muda wa Saa 9 ambao alishauri Yeye awali hasa ikizingatiwa kuwa huyu Kocha ameshacheza mechi nyingi na Timu za Kiarabu katika Klabu kubwa baadhi alizofundisha na hata Timu za Taifa hivyo nilidhani Simba SC ( Uongozi ) ungemsikiliza.
Uongozi wa Simba SC ilichokinya ni kudharau ' Utaalam ' wa ' Kiufundi ' wa Kocha Mkuu Lechantre na kuamua mechi ichezwe jioni ile ya Saa 12 ili tu wapate ' Pesa ' nyingi ambazo hata hivyo nyingi ya hizo ' Pesa ' huishia ' matumboni ' mwa wachache na kumuachia ' mzigo ' mkubwa wa majukumu ya Timu Mohamed Dewji ' Mo '.
Ni akili ndogo ilihitajika jana ambayo nashangaa Mimi GENTAMYCINE nimewezaje kuwa nayo halafu Viongozi wa juu kabisa wa Klabu yangu ya Simba ambao wana ' exposure ' kubwa na mara nyingi husafiri nchi mbalimbali duniani walishindwa kufahamu na hapa sasa ndiyo naamini kuwa kumbe unaweza ukawa Tajiri lakini ukawa ' Mpumbavu ' vile vile.
Kwa Klabu zozote zile za Afrika ya Mashariki ili kuweza kumfunga ' Mwarabu ' kama wakicheza nao huku Kwetu ni kuwalazimisha tu wacheze nao muda wa Saa 9 hadi Saa 11 tu na siyo zaidi ya hapo. Sababu kubwa ni kwamba hali ya Hewa ya Misri mara nyingi na hasa ' nyakati ' hizi huwa inakuwa kati ya Nyuzi Joto 7 hadi 11 na kuna muda inakuwa 12 hadi 15 na Wao wameshaizoea hiyo hivyo wakija huku Kwetu kwa mfano Tanzania na ukawachezesha Saa 9 hadi Saa 11 ambapo mara nyingi hali ya Hewa huwa kati ya Nyuzi Joto 25 hadi 28 na kuna muda inakuwa 29 hadi 32 unawafanya Waarabu wachoke upesi na hadi kushindwa kupumua vyema hali ambayo Kwetu Sisi huwa ni faida na tungeweza Kuwafunga magoli mengi tu.
Ili kulithibitisha hili kuwa ' mbinu ' za ' Kimafia ' huwa zinahitajika sana katika hii michuano mechi ya marudiano ya Simba SC na hawa Al Masry nimepata taarifa kwamba hii mechi itachezwa huko mjini Alexandria ambako hali yake ya Hewa huwa ni kati ya Nyuzi Joto 8 hadi 12 hali ambayo nina uhakika itatutesa sana Sisi Simba SC huko na ndiyo maana wenye akili na tunaojua mpira akina GENTAMYCINE siye tumeshajua kuwa ' Safari Imewadia ' na katika hili wala tusidanganyane. Wewe umeshawaruhusu ' Waarabu ' wakufunge hapa Kwako goli mbili ( 2 ) huku Wachezaji wao mahiri kabisa hasa Aristide Bance akiwa amepumzishwa na ameshawasoma Mabeki wote wa Simba SC unategemea nini tukienda Kwao?
Mwisho kabisa leo naonya tena kwa kusema kwamba nawaomba Uongozi wa Simba SC uache ' kumuingilia ' Kocha na hasa Benchi la Ufundi na pia Wachezaji wa Simba SC waonyeshe Nidhamu na wasikirudie tena kile walichomfanyia jana Kocha Lechantre kwa kutaka kumpinga ' maamuzi ' yake alipotaka kumtoa Winga Shizya Kichuya. Naamini huyu Beki Juuko Murshid hapangwi kutokana tu na ' Majungu ' ya baadhi ya Viongozi / Watendaji wa Simba kwa sababu zao wanazozijua Wao.
ANGALIZO
Huu ni Uchambuzi wangu wa Kimtizamo Mimi GENTAMYCINE hivyo najua kuna wale Watu ' wavivu ' wa kufanya ' analysis ' huwa wanasubiri Watu kama Sisi tuje na ' chambuzi ' zetu hizi halafu wanazinakili kama zilivyo na kuziweka katika Kurasa zao za Mitandaoni huko katika Websites na Blogs zao na kujifanya wameziandaa Wao.
Huwa mnatuvunja mno moyo kwa aina hiyo ya ' Plagiarism ' mnayoifanya Kwetu hivyo nawaombeni wale wote mtakaopenda kuchukua hii ' analysis ' ndogo tu ya GENTAMYCINE na kuitumia huko katika Mitandaoni yenu msikose tu kunifanyia ' acknowledgement ' Mimi pamoja na huu Mtandao wangu pendwa wa JamiiForums ambapo huwa napenda ' Kuutumia ' sana kuweza mawazo yangu / mitazamo yangu mbalimbali ya kuhusu nyanja mbalimbali za Kijamii, Siasa, Burudani, Michezo, Elimu, Mahusiano, Habari, Uandishi na Mawasiliano, Saikolojia na Ujasusi.
Niwatakieni usomaji mwema wa ' Chambuzi ' yangu hii.
Nawasilisha.