Simba SC inahitaji REFORMS

Megalodon

JF-Expert Member
Joined
Apr 9, 2021
Posts
3,534
Reaction score
7,866
Hilo ndio ninaloweza kusema. Tatizo hata kocha mpya haitosaidia kama itaendelea kuwa na njemba hizi hizi

Ukweli wachezaji wamechoka , hata wao hawajui tena nini cha kufanya . Wame offer all that they have. Na tukubali kuwa uwezo wao umegotea hapo.

Ukiangalia Yanga, mpira wake ……. Hata wakirudiana na SSC mara 10 , SSC bado itafungwa goli sio chini ya 5 .

Yaani SSC haina mipango endelevu, mpaka timu inafikia hatua hii. Literally tumejaza watu wa hovyo kwenye management.

SSC inahitaji reforms kuanzia management,

Benchi la Ufudi

na wachezaji.

hili la kocha ni moja Kati ya hayo manne.

Ukisolve ishu ya kocha ukaacha management na benchi la ufundi lilelile…….. na wachezaji wale wale bado hujatatua tatizo.

Ili kutatua tatizo la sasa kwa SSC. Ni lazima benchi la ufundi lisafishwe,

management isafishwe na kukwekwa vijana wenye IQ na chachu ya mabadiliko kwenye nafasi za CEO,

kusafisha wachezaji almost wote kuanzia Kennedy , chama, Mikison M Hussein, Saido , Boko , Marasta etc etc kwa sasa hawana Tena cha ku offer , wana tafuta riziki tu , we respect them but prime yao ilishaisha na tunakumbuka history zao but kwa sasa organization goals na goals zao ni tofauti….. we must accept hilo if we are to prosper

Chama bado yupo SSC kupitia background yake tu but sio kiutendaji …… mikison the same ….. Saido sijui hata aliingiaje SSC , tunaviongozi vichwa maji wasiokuwa na future wala akili , kazi kupoteza muda kwenye mitandao kwa kumtumia yule kijana wa mipasho na hashua. Investment kubwa ipo kwa social media , kwenye pitch ni mtihani

SSC ni kusajili vijana under 30 wenye kasi na nguvu kama walivofanya wenzenu Yanga.

Kuteaua independent Committee ya Scouting isiyoingililiwa na itakuwa reliable for whatever…..

tofauti na hapo mtamtafuta mchawi na hamtompata unless mkienda kumuangalia kwenye kioo ndio mtamuona.


Huwezi kutatua matatizo yale yale kwa kutumia management ile ile , wachezaji wale wale , bench la ufundi lile lile……. Never on earth [emoji290]

This time robo fainali hamtoboi

HM
 
Kwa uchungu sana, lakini ndio reality.
 
Uko sahihi Mkuu, kwa uchezaji huu kama wa Leo, mwaka huu robo hatutafika, hapa makundi ndio mwisho wetu.
Viongozi wajitathimini, wakubali kuwa wameshindwa.
 
Hakika umeneno vyema umegonga kwenye mshuno kabsa. Kwa mfano huyu CEO Mpya toka atue simba amefanya Nini cha maana ? Yani hanamipango kabsa yupo yupo tu
 
Mimi nilijua yanga wametuloga kumbe hatuna timu kabisaa yaani tumefikaje hapa? Is this Simba I was proud of ikicheza unakuwa na furaha mwanzo mwisho au naota! Hivi huyu Che Malone ndio tuliambiwa ukuta sijui wa nini,Ngoma huyu ndio aliibiwa airport au mwingine..yani butua butua tuuu .Mimi naona tujitoe tu kwenye haya mashindano tubaki ligi kuu tu tupambanie nafasi ya pili au ya tatu ili kujipanga na msimu ujao.Sijui kwa nini nijingiza kushabikia mpira daaa inauma Sana!
 
Hakika umeneno vyema umegonga kwenye mshuno kabsa. Kwa mfano huyu CEO Mpya toka atue simba amefanya Nini cha maana ? Yani hanamipango kabsa yupo yupo tu
Amefungua group la whatsapp, mashabiki wa Simba SC tutoe maoni yetu huko.
 

Mkuu Mwenye kiti Man ngugio nasikia ni Yanga Pure 110% Hayuko pale kwa ajili ya Simba!
Simba Inatakiwa Kusajili Vijana wasiozidi 3 tuu disisha dogo!
Pia Wamuachie Kocha Mpya Maamuzi yote kuhusu Wachezaji!
Kweli Wachezaji wengi ni Over 30yrs hata kama wakidanganya!
Hawa Makocha wazawa hamna kitu!
Huu ndio Ukweli Mchungu!
Kuna Baadhi wa Viongozi huwatumia Makocha wazawa kwa maslahi yao binafsi ili wachezaji wao kipenzi wapangwe!
Tz makocha wazawa Bado sanaaa,
Specifical Simba!
Eti Matolla ndio kocha Tegemeo Mzawa wa Simba[emoji30][emoji30][emoji1787]
 
Akili ileile haiwezi kutatua matatizo yaliyosababishwa na akili hiyohiyo
 
Hakika umeneno vyema umegonga kwenye mshuno kabsa. Kwa mfano huyu CEO Mpya toka atue simba amefanya Nini cha maana ? Yani hanamipango kabsa yupo yupo tu
Ameanzisha group la whatsup alafu wewe huoni alichofanya[emoji1787]
 
Wakati wa Mechi Mangungu na Jaribu Tena wameteta Muda mrefu Sana, nadhani kesho watajiuzulu.
 
Nikimtazama Luis anavyocheza nawaza Sana yatakua maajabu Kama hawataachana nae dirisha dogo.
Che Malone hakuna kitu
Kidogo ngoma.
Onana hamna kitu temeni
Kramo temeni
Chama temen
Kapombe temeni
Mzamiru temeni
Bocco tema Mara mbili
Ayubu temeni
Saidoo temeni
Kanoute temen.

Benchi la ufundi tema wote.

Viongozi tema wote rudisha Babra na vijana wapya.

Try na mangungu hata sura zao tu zinnasadifu mengi Sana hao watu.
 
Nasikia wachezaji wote wa Simba ni mashabiki wa Yanga. Yaani wapo kimwili Simba ila kiakili Yanga.
 
Uko sahihi kabisa na mimi ndiyo maana nimekuwa nasema itachukua muda mrefu sana hii timu kukaa sawa maana hata wanaotakiwa kurekebisha nao ni chanzo cha tatizo.

Kuanzia wanaohusika na usajili, management inayoendesha shughuli za kila siku za timu, timu nzima ya ufundi na kambi huko kote kumeoza. Matatizo ya uwanjani ya Simba yanaanzia kwenye uwanja wa mazoezi. Unarudi Bodi ya Wakurugenzi unakutana na kina Asha Baraka na mifumo na taratibu zilizopitwa na wakati, zilizojaa siasa na ambazo haziruhusu uwajibikaji.

Baadhi ya haya mambo nimeshayasema sana.


 
Kiukweli morali ya timu yetu ipo chini sana, pamoja na mambo mengine timu inatakiwa kujengwa kisaikolojia sana kwa sasa, tupo katikati ya msimu hatuwezi kuunda timu mpya.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…