Simba SC kiungwana toeni tamko kuomba radhi kadhia ya jana Mkapa Stadium

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2013
Posts
60,660
Reaction score
121,325
Najua baadhi ya watu (waliokutwa na tatizo) wamekereka na kukwazika na usumbufu wa kuwa na tiketi na kutoingia ndani jana Uwanja wa Taifa katika Simba Day.

Nichukue nafasi hii kuuomba Uongozi wa Simba SC kutochelewa kuwaomba radhi wahusika waliokutwa na kadhia hii.

GENTAMYCINE nashauri ikiwapendeza Uongozi wa Simba SC ufanye utaratibu maalum wa kuwajua na kujua Idadi yao kisha wafidiwe kwa kuingia bure hata mechi mbili za Simba SC na kwa wale walio mbali wanaweza kurejeshewa fedha zao.

Na katika kuomba kwao radhi huko uongozi wa Simba SC utoe ahadi kwa wadau wa michezo nchini na hakikisho kuwa kadhia hii iliyojitokeza haitokuja kutokea tena.

Poleni sana nyote mliopata kero hii.
 
Na GENTAMYCINE nashauri ikiwapendeza Uongozi wa Simba SC ufanye Utaratibu Maalum wa kuwajua na kujua Idadi yao kisha wafidiwe kwa Kuingia Bure hata Mechi Mbili za Simba SC
Labda iwe mechi ya kirafiki, lakini nyingine zote viingilio vina maslahi ya wadau wengi zaidi (TFF, BMT, DRFA nk). Kwa hiyo mechi ya ligi hakuna klabu inayoweza kujiamulia kuingiza watu bure hata kama ni mwenyeji. Kama wanaweza wasubiri ya kirafiki itakapotokea
 
Una hoja lakini hutasikilizwa.
 
Acha upuuzi wewe kwani wewe ungevaa Kama Yule ingekuwaje tungesema unadhalilishwa.kijana alikua kazini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…