Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
Kikosi cha timu ya Simba SC kinatarajiwa kuondoka nchini Jumatano alfajiri (Disemba 4) kuelekea Algeria kwa ajili ya mchezo wao wa pili wa hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika. Akizungumza kuhusu safari hiyo, Afisa Habari na Mawasiliano wa klabu ya Simba SC, Ahmed Ally, amesema kuwa wachezaji na viongozi wa timu hiyo wataelekea Algeria kwa ajili ya kukutana na wapinzani wao, CS Constantine, katika mechi ya kuwania hatua ya juu ya mashindano hayo.
Simba SC inajiandaa kwa mchezo muhimu ambapo wanatarajiwa kupigania pointi tatu muhimu dhidi ya timu ya CS Constantine, wakilenga kuimarisha nafasi yao katika kundi A la Kombe la Shirikisho Afrika.
Simba SC inajiandaa kwa mchezo muhimu ambapo wanatarajiwa kupigania pointi tatu muhimu dhidi ya timu ya CS Constantine, wakilenga kuimarisha nafasi yao katika kundi A la Kombe la Shirikisho Afrika.