Simba SC kwa mlichokifanya kwa Gadiel Michael ni Udhalilishaji, Uhuni na Tusi Kwake muombeni Radhi

Simba SC kwa mlichokifanya kwa Gadiel Michael ni Udhalilishaji, Uhuni na Tusi Kwake muombeni Radhi

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2013
Posts
60,660
Reaction score
121,325
Na kilichoniuma zaidi GENTAMYCINE ni kwamba yaani mlimchagua Mchezaji ambaye mnajua hana Nafasi Kikosini na ambaye mnamuacha Dirisha hili Dogo lijalo ili mumvalishe hili Bomu hata kama atapewa Adhabu haitokuwa na Athari kwa Kikosi kizima.

Na najua kuwa mlitumia Akili Kubwa ya Kumshawishi Beki ( Mchezaji Gadiel Michael ) afanye huo Upuuzi Usiovumilika na Kumpa hilo Jukumu la Kishirikina ( la Uvaaji Mabomu ) kwa Kumdanganya na hata Kumtishia kuwa akifanya mtambakiza Kikosini au mtamuacha mazima na kwakuwa nae anaona ni bora akae Benchi Simba SC ila alipwe hayo Mamilioni yenu ya Mshahara ili Duka lake Kubwa la Nguo lililoko Morocco ya Magomemi analouza Mkewe liendelee kuliko kwenda Kupotea katika Vilabu vingi vya Kimasikini ( Kawaida ) vya Mikoani.

GENTAMYCINE napenda mno Utani wetu wa Simba SC na Yanga SC ila kuna muda huwa naweka Utani pembeni na Kuongelea Uhalisia na Maendeleo na wala nisiwaficheni kwa hili mmenikera mno na hapa wala msidhani kuwa mliyemdhalilisha ni Yeye tu Mchezaji ( Beki ) Gadiel Michael bali mmetudhalilisha hata Sisi wana Simba SC wote na Wadau wa Soka na Michezo kwa ujumla wake hapa Tanzania.

Na kama kweli hamkuwa na nia hii ya Kumdhalilisha hivi Beki ( Mchezaji ) Gadiel Michael kwanini Jukumu hili ( hilo ) la Kipumbavu ( Kipang'ang'a ) hamkumpa Beki Tegemeo Henock Inonga au Kiungo Tegemeo Muzamiru Yassin au Mchezesha Timu ( mwenye Timu ) Clatous Chama au Mfungaji wetu Tegemeo kwa sasa Moses Phiri?

Muombeni upesi Radhi Gadiel Michael.

Cc: Ngalikihinja, Nas Mapesa
 
Na kilichoniuma zaidi GENTAMYCINE ni kwamba yaani mlimchagua Mchezaji ambaye mnajua hana Nafasi Kikosini na ambaye mnamuacha Dirisha hili Dogo lijalo ili mumvalishe hili Bomu hata kama atapewa Adhabu haitokuwa na Athari kwa Kikosi kizima.
Well said bro..Bravo[emoji119]
 
Simba ilijifanya imebadili mfumo ila upuuzi ni uleule Tena afadhali hata tulipokuwa kabla ya mageuzi
 
Wamuongezee mkataba wa miaka 2 dirisha dogo kufidia...
 
Back
Top Bottom