Simba SC Kwanza.. Mengine Baadae.

Simba SC Kwanza.. Mengine Baadae.

sembo

JF-Expert Member
Joined
May 25, 2011
Posts
4,350
Reaction score
3,451
Wanadai eti 'Uzalendo Kwanza'!!
Kwa soka lile, mipango ile, matokeo yale, kujituma kule kwa 'mapro' wetu n.k kuna Uzalendo kweli pale??
Kwangu mimi 'Simba SC Kwanza.. Mengine Baadae'. Kwanini hili??
1. Simba SC ndiyo timu pekee inayocheza soka maridadi na makini kwa sasa katika ukanda huu wa Africa mashariki na kati, pia ndiyo timu yenye wachezaji bora zaidi katika ukanda huu.
2. Wachezaji wa Simba SC wanajitoa na kujituma kwa zaidi ya 100% kwa ajili ya timu yao pendwa.
3. Katika siku za hivi karibuni, kila msimu Simba SC hatoki kapa. Mfano, msimu uliopita Simba SC alikua bingwa wa VPL, msimu huu kaanza na ngao ya hisani.. Yaani kwa kifupi lile kabati lao la kutunzia makombe ni heka heka tupu kila msimu.
4. Aina ya 'kabumbu' wanalosakata Simba SC ni wanaonana haswaa, wanazijua njia za mipira, wanacheza kwa kujiamini n.k. Kwa kifupi Barcelona ni "Simba SC ya Ulaya".

Sasa kwa mwendo huu.. Naachaje kuiweka Simba SC Kwanza halafu hayo mengine yakafuata??

NB: 21/10/2018 Simba SC atakua Taifa Stadium kupambana na timu anayoichezea Alex Kitenge, Stand United katika muendelezo wa TPL. Karibuni Taifa.
 
Simba timu yenye kikosi kipana
Screenshot_2018-10-13-02-53-09.png
 
Bringback Mo and free Haji Manara! Mko kipindi kugumu kaka lakini huachi porojo zako! Majuzi CAF walitoa orodha ya timu bora sijui mko nafasi ya ngapi?
 
Bringback Mo and free Haji Manara! Mko kipindi kugumu kaka lakini huachi porojo zako! Majuzi CAF walitoa orodha ya timu bora sijui mko nafasi ya ngapi?
Mkuu, humjui Sembo na story zake za Simba. Haoni wala hasikii lolote.
 
Aisee! Anaonekana muongo muongo hivi? Asante kwa tahadhari
 
Bringback Mo and free Haji Manara! Mko kipindi kugumu kaka lakini huachi porojo zako! Majuzi CAF walitoa orodha ya timu bora sijui mko nafasi ya ngapi?

Mkuu kutekwa kwa Mo hakuzuii shughuli zingine zisiendelee. Jambo lipo katika vyombo vya ulinzi na usalama wabalishughulikia.. Unataka sisi wanachama kindaki ndaki tufanyaje? Si jana tu tulivyokutana katika makao ya klabu tukamuombea kila siku tunafanya hili zoezi.. Unataka tufanye nini zaidi ya hili?
 
Hii ndio simba unaniekea agrey Morris, mudathiri, mwantika, ulimwengu, kessy, himid mao wacheza ndondo kweli Tanzania tumelaaniwaga tena nazani walikula ubwabwa maana walikua mrenda sana
 
Hii ndio simba unaniekea agrey Morris, mudathiri, mwantika, ulimwengu, kessy, himid mao wacheza ndondo kweli Tanzania tumelaaniwaga tena nazani walikula ubwabwa maana walikua mrenda sana
Mkuu kwa hii ya Taifa Stars michuano ya AFCON na WC tutaendelea kuitizama katika kideo kwa miaka mingi ijayo.
 
Mkuu kutekwa kwa Mo hakuzuii shughuli zingine zisiendelee. Jambo lipo katika vyombo vya ulinzi na usalama wabalishughulikia.. Unataka sisi wanachama kindaki ndaki tufanyaje? Si jana tu tulivyokutana katika makao ya klabu tukamuombea kila siku tunafanya hili zoezi.. Unataka tufanye nini zaidi ya hili?
Anataka tujikamue uhai labda,la Manji alifurahia,la Lissu halikumuhusu,Azory hakumfahamu Wala Ben Rabiu wa Saanane.Yeye ameona la Mo.
 
Mnajituma 100% alafu mnachapwa na mbao ya mgongo ambao wanajituma 40%
 
Simba ni litimu la makanjanja lililo anzishwa na mganga wa kienyeji mwanamke, mafanikio siruri ingawa washabiki wake wanapiga domo la hatari
 
Simba ni litimu la makanjanja lililo anzishwa na mganga wa kienyeji mwanamke, mafanikio siruri ingawa washabiki wake wanapiga domo la hatari
Hao ndugu akili zao zote kazibeba Manara wamebaki vichwa vitupu..ndiyo maana mambumbumbu fc
 
Simba ni litimu la makanjanja lililo anzishwa na mganga wa kienyeji mwanamke, mafanikio siruri ingawa washabiki wake wanapiga domo la hatari
Simba inajua kucheza mpira wa mdomoni
 
Back
Top Bottom