Simba SC leo dhidi ya Namungo FC tumalize shughuli ndani ya '90 minutes' kwani tukienda 'Matuta' tunatolewa, hatuna akina Vicent Aboubakar wengi

Simba SC leo dhidi ya Namungo FC tumalize shughuli ndani ya '90 minutes' kwani tukienda 'Matuta' tunatolewa, hatuna akina Vicent Aboubakar wengi

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2013
Posts
60,660
Reaction score
121,325
Katika hili wala tusifichane Simba SC ya sasa haina Wapiga Penati na hata Wapiga Faulo mahiri (kama Vicente Aboubakary wa Timu ya Taifa ya Cameroon) na Wachezaji walioko wameshatuthibitishia hilo kama Bwalya Rally na Nyoni Erasto.

Hivyo basi kuelekea mtanange Wetu wa leo Usiku Mapinduzi Cup dhidi ya Namungo FC naomba mkakati uwe ni kumaliza Shughuli ndani ya dakika Tisini (ninety minutes) tu ila kwa Uwezo mdogo wa Upigaji Penati walionao Wachezaji wetu naogopa tukienda nao Matuta ( Penati ) Simba SC tunatoka (tunafungwa)

Otherwise GENTAMYCINE nawatakia tu Ushindi Azam FC kwani kuna Watu kuelekea Michuano hii walitoa Kashfa sana kuwa Wachezaji Wao mahiri na Waandamizi hawatocheza Kombe hili lisilo na Hadhi ila Juzi na Jana walikuwa busy kusafirisha hao hao Wachezaji Kisiwani Zanzibar ili leo waokoe Jahazi kudadadeki.
 
Kocha Ni wakuchunga Sana hasa upangaji wake wa kikos huko Zanzibar Ni wa mashaka Sana ,pia Ni mgumu kufanya sabab ,yeye sab zake Ni kuanzia dakika ya 60 huko kitu ambacho Ni hatar ,Namungo Ni wazuri pia Wana benchi jipya la ufundi hivyo Pablo akae chonjo Sana.

Hili lipo Waz Simba akikubali draw ndan ya dakika 90 ashaaga mashindano.

Wachezaj wa Simba wakumbushwe swala la kucheza na majukwaa leo lisiwepo wacheze mpira wapambanie nembo ya club ,baada ya ushindi hizo sifa wanazozitaka watazipata mpaka watashindwa pakuziweka.

Nidhan ,kujituma ,kupress muda wote ,kukaba ,back pass zisizo na ulazima Leo zisiwepo kabisa.
Leo wavuje jasho kweli kweli maana wanaoumia Ni sisi mashabik na sio hao wachezaji sisi ndio tunapata taabu huku mitaan .
Mechi za majaribio zimeisha kocha na benchi la ufundi wawe serious ,ninge huja baada ya kupoteza.

Nawatakia ushindi mzur Wana Lunyasi na tuseme tutashinda kwa uwezo wa mungu jumrisha na juhudi za wachezaji wetu.

Note: Morrison ,mhilu,mwenda,Gadiel,Bocco,moukolo ikiwezekana wasiwepo hata sab.
 
Katika hili wala tusifichane Simba SC ya sasa haina Wapiga Penati na hata Wapiga Faulo mahiri (kama Vicente Aboubakary wa Timu ya Taifa ya Cameroon) na Wachezaji walioko wameshatuthibitishia hilo kama Bwalya Rally na Nyoni Erasto.

Hivyo basi kuelekea mtanange Wetu wa leo Usiku Mapinduzi Cup dhidi ya Namungo FC naomba mkakati uwe ni kumaliza Shughuli ndani ya dakika Tisini (ninety minutes) tu ila kwa Uwezo mdogo wa Upigaji Penati walionao Wachezaji wetu naogopa tukienda nao Matuta ( Penati ) Simba SC tunatoka (tunafungwa)

Otherwise GENTAMYCINE nawatakia tu Ushindi Azam FC kwani kuna Watu kuelekea Michuano hii walitoa Kashfa sana kuwa Wachezaji Wao mahiri na Waandamizi hawatocheza Kombe hili lisilo na Hadhi ila Juzi na Jana walikuwa busy kusafirisha hao hao Wachezaji Kisiwani Zanzibar ili leo waokoe Jahazi kudadadeki.
MTANIiiiiiii, hutajia hujui Bwege wewe.. Sasa ulitaka wasije... Kombe lazima tuchukuwe tu
 
Kila la heri Namungo FC! Ni wakati wenu huu sasa wa kulipa fadhila kwa Mbunge wenu wa Ruangwa Mh. Kassim Majaliwa, ambaye kimsingi ana mchango mkubwa sana wa kuwafikisha hapo mlipo.
 
Back
Top Bottom