Simba SC mmeanza pamoja na mmalize pamoja

moodykabwe

JF-Expert Member
Joined
Aug 16, 2015
Posts
625
Reaction score
602
Kwanza kabisa nianze kuwapongeza kwa mwendelezo wa matokeo mazuri katika michuano ya Klabu Bingwa barani Afrika hatua ya makundi na mapaka sasa mpo kileleni na jumla ya alama 10.

Sisi wadau kwa pamoja tunaamini huu ndio uwezo wenu halisi na ile sare yenu dhidi ya Tanzania Prisons haikuwa sawa kwani Prisons watakuwa waliwafitini mahali, hamuwezi kuwa kikosi kamili halafu wajelajela wapo pungufu kwa zaidi ya dakika 50 halafu mwishowe nyie ndiyo mchomoe tena kufuatia saa ya mwamuzi kupoteza majira kwa bahati mbaya.

Tunaamini Uwepo wa paka na mambo mengine yanayojitokeza kwenye mechi zenu ni mizengwe tu ya wapinzani wenu kwani mpo vizuri kimaandalizi na tunajua si muda mrefu shambuliaji la Dunia Junior Lokosa atazikosha na kuzikonga nyoyo zenu.

Tunaamini hata baada ya kumaliza michuano hii hatutasikia maulizo juu ya Bilioni 20 kwani maandalizi na ushindi unaopatikana sasa ni matunda ya zile Bilioni 20 ambazo mwekezaji anazitoa huku akiandika kwenye note book yake.

Tunaendelea kuamini kuwa baada ya mafanikio haya Mwenyekiti mliyemchagua ataitisha mkutano mkuu na kuwasomea mafanikio ya nje ya uwanja hasa yale ya kiuchumi aliyoyafanya mwekezaji kwa uwekezaji wa hisa asilimia 49.

Tunaendelea kushawishika kuamini kuwa baada ya furaha hii ya kipindi hiki utadhani wana wa Israel walipokuwa wanavuka bahari ya shamu,tutaona faida mliyopata kutokana na uwekezaji wa wanachama kwa umiliki wa hisa asilimia 51 walionao kwenye klabu.

Hatuwezi kuchoka na tutaendelea kuamini kuwa si muda mrefu upande wa Simba Sports Club na wala sio Simba Mo Sports Club utawaambia wanachama wake namna ya kutumia mpunga uliopatikana kutokana na makampuni zaidi 7 ya Mo kuitumia nembo ya Simba.

Tutaendelea kuwaunga mkono na kuwaamini kuwa baada ya kumalizika kwa furaha hii viongozi wote mlionao katika Simba 5 mlizonazo watakuja na majibu mujarabu juu ya yala maswali mliyoulizwa na tume ya ushindani FCC na kutakiwa kuyatolea majibu ili muendelee kumalizia ndoa yenu na mwekezaji wenu.

Tunafurahi na kuzidi kuwaamini endapo Uongozi wenu utawajulisha kuwa uliuza jezi kiasi gani kwa aina zote zaidi ya [emoji2393] mlizonazo huku mkiambiwa wazi mgao wenu ni upi kwenye kila jezi moja iliyouzwa.

Tutaendelea kuamini ule mpango wa kitengo chenu cha Kurugenzi ya Mashabiki ambao ulianzishwa sasa utakuwa na majibu juu ya idadi ya wanachama wapya waliopatikana na kiasi kilichovunwa kwakuwa Simba ni Next Level.[emoji1480][emoji1480]

Tunaamini kabisa kuwa baada ya ukimya wa mzee Kilomoni na hoja zake hata akirudi kesho tayari viongozi wenu watakuwa na majibu ya kukata kiu zenu kwani tayari wameseti mambo kuwa sawa.

Mwisho lakini siyo kwa umuhimu tutafurahi na kuamini kuwa Madam Bidada CEO atakuwa amekamilisha sehemu kubwa na ziara zake na picha alizopiga huku akija na mafanikio aliyoyapata kwenye ziara zake,yawe manufaa ya Klabu au yake binafsi mana wahenga walisema mtembea bure ni tofauti na mkaa bure.

Wote tunajua nyimbo nzuri ni ile yenye kiitikio

Msemakweli wa haki

Nimemaliza
 
Sisi mashabiki tunachotaka ni ushindi tu. Hayo yote uliyoandika hayana tija kabisa umeandika matope matupu..
 
Kwa umoja wetu hadi Ubingwa(VPL). Hadi Nusu fainal (CL)
 
"Mwisho japo si kwa umhimu, suala la nani anaimiliki Simba halina mashiko kwa mpenzi wa Simba kikubwa ushundi na mataji vipatikane. Timu zote dunia zinazofanya vizuri zinamilikiwa na mtu mmoja au wachache, na hao ndo wanaonufaika na timu kifedha wengine tuliobaki tunafurahia ushindi basi. Kama Mo anaimiliki Simba wewe mshabiki wa Mtwara, Vyawa, Kasulu n.k unapata hasara gani kama timu inafanya vizuri?"

Copied and pasted from K11
 
MAFANIKIO HAYAJI KWA KULALA[emoji16][emoji16][emoji16].
simba inapata wanachostahili.
Sababu wamewekeza .
yanga ligi ya mabingwa sio rahisi kama mnavyoona simba wakishinda.
NI MIPANGO
 
Unateseka kutokea wapi bro? Sie kama mashabiki tunachotaka ni timu kufanya vizuri na timu inafanya vizuri. Period.
 
Unateseka kutokea wapi bro? Sie kama mashabiki tunachotaka ni timu kufanya vizuri na timu inafanya vizuri. Period.
Huyu ni utopolo wa damu!! Amejaribu kujificha lakini harufu ya utopolo imemuumbua!
 
Achana na sisi kabisa wewe mtopolo
 
Mtoto wa kiume unauza makalio JF ni laana hoyo.
Endeleeni kutengeneza vyumba vya futi 3 hapo vidimbwini sie tunasonga mbele na tunaongoza kundi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…