Simba SC mnalijipa hukumu gani baada ya madudu mliofanya kwenye usajili wa Yusuph Mhilu

Simba SC mnalijipa hukumu gani baada ya madudu mliofanya kwenye usajili wa Yusuph Mhilu

Kichwa Kichafu

JF-Expert Member
Joined
Apr 13, 2017
Posts
44,855
Reaction score
189,385
Habari.

Hizi habari naona Simba SC wanazichukulia poa sana kwa haya madudu waliyofanya juu ya mchezaji wa Kagera Sugar, Yusuph Mhilu.

Wamemsajili na kumtambulisha kabisa kwa wanachama wao wote kupitia social media kama walivyofanya kwa wachezaji wao wengine.

Japo Yusuph Mhilu bado ana mkataba wa mwaka mmoja katika timu yake ya Kagera Sugar, sasa tunafahamu sheria zipo wazi kabisa kuzungumza na mchezaji ambaye bado ana mkataba na timu nyingine.

Sasa naona mnajitekenya wenyewe kwa madudu haya na baadhi ya viongozi wenu kujisahaulisha na kuona ni jambo dogo sana.

Haya sisi yetu macho kuona mambo yatakavyo kwenda katika ardhi ya Tanzania chini ya uongozi wake wa TFF.

Hivyo basi tunawauliza Mwana msimbazi mnajipa hukumu gani kwa madudu haya mliyofanya kabla ya Sheria tunazozifahamu kufata mkondo wake msimu 2021/2022?

Nawasilisha Mzee Mkoloni.

Cc: Kichwa Kichafu
 
Na wamemtuma aende TFF akaombe namna ya kuvunja mkataba wake na Kagera

Nashindwa kuelewa uweledi wa klabu ya simba uko wapi hapo?

Na kwasababu TFF favor side yake ni simba basi yatafanyika magushi na kuonekana mchezaji ni mali ya simba
 
... Wamemsajili na kumtambulisha kabisa kwa wanachama wao wote kupitia social media kama walivyofanya kwa wachezaji wao wengine. Japo Yusuph Mhilu bado ana mkataba wa mwaka mmoja katika timu yake ya Kagera Sugar, sasa tunafahamu sheria zipo wazi kabisa kuzungumza na mchezaji ambaye bado ana mkataba na timu nyingine....
Unapoteza muda bure, Mhilu ameongea, amesaini na ametambulishwa Simba kabla hajamalizana na Kagera Sugar, lakini mwisho wa yote ataenda Simba na viongozi wa Kagera Sugar hawatalalamika tena ila wewe na wenzako wa aina yako ndio mtabaki na malalamiko yenu ya kanuni. Ruksa povu, ruksa kununua kesi ya Kagera Sugar
 
Namuona tu huyo Yusuph Mhilu akirejea nyumbani baada ya miaka miwili kuisha. Bila shaka amefanya tu makusudi kwenda kuishi na wazazi wa kufikia baada ya kuona wazazi wake halisi wanamchukulia poa poa!
 
Mimi nimemsikiliza Farhan Kiamu yule mchambuzi wa michezo Clouds, alisema amelifatilia hilo suala na kilichotokea ni hiki, nanukuu

"Simba walimalizana na Muhilu na walikua tayari wamewasiliana na Kagera Sugar na offer ya usajili ilikua imekubaliwa na pande zote mbili

Lakini walipokua hatua ya mwisho ikaja kugundulika kuwa kwenye mkataba wa Muhilu kuna kipengele kinachosema kama unataka kumchukua mchezaji huyu inabidi uchukue mshahara wa Muhilu uuzidishe mara muda wa mkataba uliobakia na timu ya Kagera,

So walipochukua mshahara wa Muhilu anaoupokea Kagera wakazidisha mara 12 (mwaka mmoja) ikaonekana pesa ni ndogo tofauti na kiasi walichokubaliana na Kagera ili wauvunje mkataba, so simba wakaona walitaka kupigwa na ndipo hapo wakasimama na mkataba unavyosema

Kitu hicho kikafanya kutokuelewana kati ya viongozi wa kagera na Simba ndio maana kagera wameamua kuja kutafuta public sympathy ili wasaidiwe na nguvu ya umma" mwisho wa kunukuu

Ila yote kwa yote Simba bado wanaingia matatizoni maana walikosea kumtangaza mchezaji bila kukubaliana na timu aliyotoka
 
Utopolo tulizeni makalio, ligi bado haijaanza tayari mayowe kibao, na safari tutawadhalilisha na hiyo mishikamoo jazz yenu ya kikongo.
 
Utopolo nendeni CAS wawape ubingwa Mhilu kasainiwa kijanja janja.
 
Back
Top Bottom