Nakubaliana na wewe iendelee kubaki na nyota wake, lakini je ikitokea timu ikamuwekea Luis dau la mshahara milioni 70 kwa mwezi, je simba inao uwezo huo kwa sasa kumlipa hizo 70, kifupi hakuna mkataba wa kazi ambao hauna kipengele cha kuvunjwa. Nakubaliana na wewe ushauri uliotoa wa usajili wa Djuma na Kikasa, Simba inatakiwa kuwatoa Mugalu, Kagere, Wawa na Kahata, lakini Chikwende abaki. Simba kama inaweza kuvunja mikataba ya Mukoko na Dube basi iwachukue kuimarisha timu. Muduwa sijui kiwango chake hivyo siwezi kushauri abaki au aondoke.