Simba SC na Yanga SC, zinatukwamisha

Simba SC na Yanga SC, zinatukwamisha

nditolo

JF-Expert Member
Joined
Jul 2, 2011
Posts
3,731
Reaction score
4,271
Malawi hakuna club kubwa kama Simba SC

Wala hakuna club yenye mashabiki wengi kama yanga.

Lakini team Yao ya taifa imefanya kitu kikubwa sana AFCON 2022

Team hizi nilizozitaja zinatukwamisha.

Hapo chini ni comments za mashabiki wa the flames " team ya taifa ya Malawi" kuipongeza team Yao.

Pia hata democrasia wako mbali sana kuliko sisi hapa Tanzania.
Screenshot_20220130-001549.jpg
Screenshot_20220130-001617.jpg
 
Kuharibu kivipi? mbona hujaelezea vizuri kwani Taifa star mala ya mwisho wamefanya vibaya?
 
Fafanua Simba na Yanga wanaharibu vipi soka letu?
Kuna nchi za Africa zinashiriki AFCON mpaka kombe la Dunia na zina timu za watani wa jadi kama Simba na Yanga kwa hapa Tanzania.
 
Sema tu Yanga utakuwa umeeleweka, kwa nini unataka kuiingiza Simba kwenye ujinga isiohusika.
 
Fafanua Simba na Yanga wanaharibu vipi soka letu?
Kuna nchi za Africa zinashiriki AFCON mpaka kombe la Dunia na zina timu za watani wa jadi kama Simba na Yanga kwa hapa Tanzania.
Sisi team zetu hazina team za vijana ambazo kwa ukongwe wao ingekuwa ndio chemichemi ya vipaji lakini wapi.
 
Yanga na Simba ndio zinazuia kuwa na wachezaji wengi wa Kitanzania wa kulipwa...?

Simba na Yanga ndio zinazuia kuwa na shule za watoto wadogo...?
 
Ungesema Simba na Yanga hazijatumika vizuri katika kuuendeleza mpira wa Tanzania ungeeleweka. Kuwa na vilabu hivi viwili ingekuwa ngazi muhimu ya kufikia maendeleo ya michezo na uchumi, bahati mbaya Taifa letu viongozi ndio hivyo tena. Kwa ufupi ni kama mchicha ulio ota pembezoni mwa ukuta wa choo cha shimo.
Kila nchi ingependa kuwa na Simba na Yanga.
 
Back
Top Bottom