sembo
JF-Expert Member
- May 25, 2011
- 4,350
- 3,451
Japo timu ya Simba SC imekua na kauli mbiu mbali mbali na majina ya utani kama "Simba Taifa Kubwa", "Wekundu wa Msimbazi", "Simba 5-0".. kauli mbiu kuu ya Simba SC ni "NGUVU MOJA".
Ukiiangalia timu katika misimu mitatu iliyopita, "NGUVU MOJA" tuliokua tumeizoea ilikua imepotea, timu ilikua inachechemea sana.
Msimu uliopita, kundi la Friends Of Simba lilishika hatamu klabuni kupitia memba wake wa muda mrefu, Evance Aveva. Mwanzo ulikua mgumu sana, na wote tuanafahamu kilichojili.. Na hii ilitokana na makovu yaliyoachwa na uchaguzi.
Lakini sasa ile NGUVU MOJA nilioizoea kuiona kutoka kwa "Wekundu wa Msimbazi" inarejea kwa kasi ya ajabu: Hebu cheki ilivyolejea,
1. Nguvu Moja: Katika Uongozi.
Hali sasa ni shwari katika Uongozi.. na hii haikutokea hivi hivi, viongozi waliitofautiana walikaa chini na kumaliza tofauti zao. Utulivu uliopo umesababisha uongozi kupata mda wa kubuni mambo mbalimbali yenye manufaa kwa timu, badala ya kudili na migogoro.
Mfano, kuzindua website, kuuza jezi online, bima kwa kila mwanachama, kuleta makocha bora kabisa ambao levo zao ni kufundisha ndimu zinazoshiriki UEFA champions Legue.. n.k. Yote haya ni matunda ya "NGUVU MOJA" iliyopo katika uongozi.
2. Nguvu Moja: Katika Kikosi.
Baada ya Kocha mwenye Leseni A toka UEFA, kutua Simba SC.. Umoja katika Kikosi hatimae umerejea tena. Mambo sasa yanaendeshwa kitaalamu zaidi.. Mda wa mazoezi, kikosi chote kinakua uwanjani, hakuna anayechelewa.. Mda wa kula wachezaji wote wanatakiwa kuwa mezani wakipata msosi..n.k.. Hii imefanya kikosi cha Simba kiwe zaidi ya Familia.
Ule "Ufalme" waliokua nao baadhi ya wachezaji msimu uliopita, ndani ya Simba SC hii ya Kerr hilo halipo.
Uwe ni mkongwe kama Mgosi, au kinda alfu Mgeni kama "Winga wa Ulimboka" Emanuel Ntinde wote ni sawa Hii imerejesha "NGUVU MOJA" katika kikosi.
3. Nguvu Moja: Ndani ya Uwanja.
Wahenga wana msemo mmoja kua, "Mzigo mzito mpe Msukuma akubebee".. msimu uliopita Emanuel Okwi alikua Msukuma wetu. Baada ya Kocha bora kabisa mwenye Leseni A toka UEFA kutua.. ule mzigo aliokua anaubeba Okwi (msukuma wetu) sasa umegawanywa kwa kila mchezaji.. soka linalotandazwa sasa ni Box 2 Box. Tunashambulia kama nyuki na kulinda lango kwa pamoja na kwa umakini mkubwa mithili ya Special Unit wa North Korea, wanaolinda mpaka wao dhidi ya South.
Hii imesababisha sasa kila mchezaji kua mfungaji na pia mlinzi Mf. kwa mechi NNE zilizopita Maguli, Ajibu, Kiiza, Mgosi, Banda, Isihaka, Mgimwa na Samir walitupia kambani.. na pia timu imefungwa goli moja tu tena la offside.
Hii inaonesha hata ndani ya uwanja kuna "NGUVU MOJA".
Sasa "NGUVU MOJA" inarejea kwa spidi ya ajabu (zaidi ya speed of light).. Mtaa wa pili mjipange vyema, maana huu moto hakuna wa kuuzima.
Simba SC of 2011/2012 a.k.a "The Invincible" Is Back.