GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 60,660
- 121,325
Tukishinda itakuwa ni furaha kubwa kwangu, ila kwa mazingira ya huu mchezo na mikakati fulani fulani naiona ni mechi ngumu kwa Simba SC, hadi kuhisi kuwa tunaweza kutoka sare, suluhu au hata kufungwa pia na Dodoma Jiji FC kama tusipojipanga vyema ndani na nje ya uwanja.
Kwanini GENTAMYCINE nina hofu?
Dodoma Jiji FC ni Yanga B na 98% ya viongozi wake waandamizi kuanzia Mbunge na Naibu Waziri Mavunde ni wana Yanga SC lia lia kabisa.
Hivyo GENTAMYCINE najua hawa waandamizi wa Dodoma Jiji FC wenye DNA ya Yanga kwa Kushirikiana na matajiri wa GSM watawatia sana ndimu (Morali) wachezaji wa Dodoma Jiji FC ili wafike, wagongane mno na hata kutuumizia wachezaji wetu muhimu na mahiri Simba SC.
Pia kutokana na mechi kubwa ya Klabu Bingwa wikiendi ijayo na Waangola, upo uwezekano wachezaji wa Simba SC wakacheza kwa tahadhari na uwoga wa kutokuumia ili wasiikose hiyo mechi, hivyo kufanya timu ikose matokeo leo dhidi ya Dodoma Jiji FC.
Ombi,
Benchi la ufundi litulie mno leo katika kupanga kikosi cha kucheza na wahakikishe wachezaji wanaimaliza mapema hii mechi kwa kufunga magoli mengi, ili kipindi cha pili wale wachezaji muhimu na tegemeo kwa michuano mikubwa na migumu ya kimataifa, akina Phiri, Inonga, Chama, Okra na Kanoute wapumzishwe.
Tusiende na matokeo yetu leo.
Cc: SN.BARRY