Simba SC tuliyataka wenyewe hivyo acheni tu yatupate ili tukome na Siku zingine tujifunze na muwe mnachukua Ushauri tunaowapeni

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2013
Posts
60,660
Reaction score
121,325
Yanayotokea sasa wenye ' Kuujua ' zaidi Mpira tuliyategemea ila tatizo la wana Simba SC na baadhi ya Viongozi mna dharau Kubwa mno hasa pale mkiona Watu kama akina GENTAMYCINE na wengineo wanawapeni Mawazo bora tu na Kujenga ila kwakuwa Sisi wengine siyo Watu wa ' Kujipendekeza ' Kwenu mnatuona ' Wapuuzi ' na hatujui chochote.

Kama leo Uongozi na Kocha unalalamika kuwa Ratiba zimebana hivi Kipindi kile tunacheza Mechi zile za Klabu Bingwa Afrika na tukawa tunakaa Siku 8 hadi hata 10 kama si 14 tungekuwa tunacheza Mechi zetu za Ligi hata Moja Moja tu hapo katikati leo hii hizi ' Fatigue ' zinazowakumba Wachezaji Wetu zingetokea?

Najua kwa hizi Mechi mbili hasa ile ya ' Wabaya wetu wa Msimu ' Kagera Sugar na hii ya leo ya Azam FC moja ya sababu Kubwa ambayo ni ya Kiufundi pia ni kwamba hatujacheza vyema kutokana na Changamoto kubwa ya Hali ya Hewa kwa sasa hasa katika Mkoa huu wa Dar es Salaam ila nina uhakika kama kusingekuwa na hizi Mvua Kubwa basi Wachezaji wetu wangeweza Kucheza Mpira mzuri tu ambao unajulikana na tumeuzoea kuliko huu wa leo na ule wa Juzi ambapo Timu haikucheza vizuri.

Nimeona mahala katika ' Twita ' Akaunti ya Kocha Wetu anaanza Kuja na Visingizio vingi ambavyo nikiri kuna vingine vina Tija / Mantiki ila kuna hiki kimoja kuwa Wachezaji hawachezi vizuri kwakuwa wako katika Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan ambacho napingana nae. Hivi ni Klabu ya Simba tu pekee Tanzania nzima ndiyo yenye Wachezaji wa Kiislamu waliofunga? Mbona kuna Timu zimeshinda Mechi zake japo nazo pia zina Wachezaji wa Kiislamu na wamefunga?

Na katika hili wala tusiwajumuishe sijui TFF au Yanga SC au ' Hujuma ' dhidi yetu bali ukweli utabaki pale pale kuwa Dharau zetu, Kujiamini ' Kipumbavu ' kuwa tunaweza Kucheza ' Viporo ' vyetu ' back to back ' huku tukiwa hata hatujaangalia upande wa Pili wa Kiufundi ambao ndiyo muhimu. Hapa tulikurupuka hivyo tukubali tu makosa kwa nia ya Kujijenga zaidi kwa Msimu ujao kama tutabahatika Kutetea tena Taji letu hili.

Yaani ' Kiufundi ' tunawatesa na kuwamumiza mno Wachezaji Wetu kwa kuwacheza hizi ' back to back ' na sishangai ndiyo maana hata wengi Wao sasa ni Majaruhi japo Uongozi wa Simba SC mnaficha lakini Sisi akina GENTAMYCINE ambao tupo karibu sana na hao Wachezaji Wenu tunalishuhudia hili. Na hata ikitokea Simba SC tukatetea huu Ubingwa Wetu naomba muwape Zawadi Kubwa mno hawa Wachezaji Wetu wa Simba SC kwani kiukweli kwa jinsi Ratiba ilivyo na wanavyohenyeshwa nayo ila bado wanapambana kadri wawezavyo kwa ajili ya Heshima ya Klabu yetu.

Mimi ni Mwenzenu tena kwa 100% ila leo nimeona niwapeni huu Ukweli Mchungu na naomba hili Kosa lisije likajirudia tena huko mbeleni. Bado kwa Kikosi chetu Imara na Kili\chosheheni vyema tu ( Depth of Squad ) bado Simba SC tulikuwa na uwezo wa Kucheza mechi zetu za Ligi Kuu ya Tanzania ( TPL ) vizuri sana tu bila hata Kutuathiri katika Michuano ile ya ' Champions League ' tuliyokuwepo ila tulilewa ' Jeuri ' yetu na ' Kiburi ' Kingi kuwa Sisi ndiyo kila Kitu hapa Tanzania tukasahau ya kwamba hata Timu zingine nazo zinautaka Ubingwa huu huu na zingine nyingi zinapambana kutokushuka Daraja hivyo ' its so obvious ' kwamba na zenyewe zikiwa zinacheza na Simba SC zitakuwa zinakaza / zinabana sana hali ambayo inaweza ikatupa Sisi ugumu na kushangaa hawa hawa Yanga SC ' tunaowadharau ' leo wakaja kuwa Mabingwa kwani hata Kimahesabu nao bado ni ' Title Contenders ' na lolote linaweza Kutokea na tukaja Kuumbuka na Kuficha Sura zetu.

Yangu ni hayo tu na kama nitakuwa nimewakwaza wana Simba SC Wenzangu naombeni Radhi ila GENTAMYCINE ANTIBIOUTIQUE Mimi huwa napenda mno kuwa Mkweli hivyo mnivumilie tu lakini nina uhakika mkiyazingatia haya ninayowaambieni hapa, kutafakari na kuyafanyia Kazi yanaweza yakawa na msaada mkubwa sana Kwenu. Msikate tamaa bado tuna 98% za Kuwa Mabingwa ila cha Msingi tu jitahidini Kuwajenga Kisaikolojia Wachezaji Wetu kwani naanza kuona wengi Wao sasa wana ' Presha ' na ' Concentration ' yao pia imeshuka kwa Mechi za hivi karibuni.

Nawasilisha.
 
Mmeanza sasa kuzozana wenyeww sio Simba wala yanga
 
Viporo vimekuwa vingi mpaka mnavimbiwa na mnalishwa mpaka vilivyochacha ona mnavyohara
 
Lakini wasilaumiwe sana Simba hata wangefanyaje wasingeweza kukwepa msongamano wa mechi za viporo kutokana na sababu zilizonje ya uwezo wa timu. Angalia makombe ambayo Simba ameshiriki na idadi ya mechi kwenye mabano;

1. Ngao ya Jamii (1)
2. Ligi Kuu (33)
2. Mapinduzi (7)
3. Spotipesa (3)
4. Shirikisho (1)
5. Klabu bingwa Africa (12)

Hadi sasa Simba wamecheza jumla ya michezo 57 za ushindani katika kipindi cha majuma 37 amba ni sawa na mechi 1 kila baada ya siku nne!!! Ongeza na ratiba ya usafiri katika mechi zinazohusu usafiri unaweza kuona jinsi gani mambo yalibana

Hapo hapo kuna international breaks kadhaa wachezaji wanajiunga na timu za Taifa, unaona jinsi mambo yalivyotight.

Upangaji wa ligi wa mtindo wa kucheza weekend hadi weekend kwa karibu miezi 3 ya mwanzoni mwa ligi ndio tatizo kubwa.
Ilipofika mwezi February na Machi hata kama Simba wangelazimisha isingezidi mechi 2 hadi 3 ndio wangecheza.

TFF na Bodi ya Ligi wajifunze kwa changamoto za mwaka huu angalau katika miezi ile
 
Simba itachukua ubingwa saa nne Asubuhi muda si mrefu. Hata Yanga wanalijua hilo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…