Simba SC tumuwahi Makambo kabla ajasainishwa Yanga SC

Simba SC tumuwahi Makambo kabla ajasainishwa Yanga SC

demigod

JF-Expert Member
Joined
Jan 2, 2015
Posts
8,292
Reaction score
15,250
Viongozi wetu wanafanya kutwanga maji kwenye kinu hivi sasa. Maana usajili wa msimu huu haionekani kuponesha vidonda vya mabao matano matano tuliyoyapata msimu uliopita wa klabu bingwa afrika.

Ninaona tunaacha kusajili high profile player, badala yake tunasajili washika pembe tu. Kila siku wanasajiliwa Mabeki na viungo. Hivi hamuoni tatizo kuwa tunashindwa kupata magoli kwenye mechi za ushindani?

Nasikia Eng Hersi atatua Lubumbashi jioni hii kufanya mazungumzo na Makambo ambaye amesalia miezi 6 kutamatisha mkataba wake na Horoya AC.

Kwanini tusihakikishe tunafanya umafia na sisi ili tuongeze makali pale mbele?
 
Hii ngedele mpaka sasa ndan ya masaa 2 imeanzisha nyuzi 10 za kuihusu simba ,,subr mafungu mafungu ya wachezaji wanatua Leo na tapeli kutoka GSM
 
Safari hii tunawachezea Akili tutakavyo. Tunatema mate kulia halafu tunafukia kushoto
 
Leo tumesajili beki kisiki anaitwa bwana Ame. Ni mzuri kuliko mabeki wote hapa nchini. Simba nguvu moja
 
Hamna timu itakayoweza kumnunua Makambo. Si Yanga wala Simba, msijipe moyo .
 
Hamna timu itakayoweza kumnunua Makambo. Si Yanga wala Simba, msijipe moyo .

Na umasikini wa Yanga ulivyo waliweza kumchukua Senzo, kwanini Simba tushindwe kwa Makambo?
 
Kupola ndio nini sasa? Kajifunze kiswahili.

Mkuu sikusoma na wala sikutaka kukisoma kiswahili kwakuwa ninakichukia mno aisee.

Sikuona namna yeyote ya kuwa kingeweza kuniletea Ugali sebuleni kwangu.
 
Hahaaa hivi kumbe ni kweli simba hawana scouting team, mnavizia yanga anataka kusajili nani, ndo mnamuwahi nyie fasta na dau kubwa la hela.

Bila yanga nyie hamna kitu, shukuruni Yanga hana hela
 
Na umasikini wa Yanga ulivyo waliweza kumchukua Senzo, kwanini Simba tushindwe kwa Makambo?
Kwani wewe unayo hela ya kumchukua? Au kuna mtu unamtegemea amchukue kwa hela yake?
Maana unaposema "tushindwe" sielewi wewe na nani.
 
Back
Top Bottom