Laki Si Pesa
JF-Expert Member
- Dec 20, 2018
- 5,085
- 9,022
Kotei na Okwi hawakuuzwa, mikataba yao iliisha na Simba hawakuwa na uwezo wa kufikia dau.Simba walikosea kwenye usajili wamemuuza kotei Hadi sasa hiv pengo lake linaonekana kotei alikuwa mnyama ana nguvu anakaba kwelikweli aliziba udhaifu wa mabeki wa Simba ukiangalia kwa team ya Simba ya sasa mtu Kama huyu hawana.Kiufupi team aipo balance wanawachezaji wengi wakuchezea mpira wakabaji hawana mkude na fraga sio defensive midfielders Bali both ni holding midfielders.
Kosa lingine ni kumuuza okwi bila kuleta mtu sahihi wakuziba pengo lake Kama Kagere akiwa afungi okwi anatupia mpaka okwi anaondoka alikuwa mfungaji wa pili wa Vodacom premier league viongozi wa Simba wakamleta yule striker garasa wa kibrazili.Kingine msimu uliopita Simba walikuwa na tatizo la mabeki nilitegemea wakamleta mtu sahihi Kuna yule beki number 5 wa nkana ni bonge la beki lakini hajamsajili wameleta magarasa.
Kosa lingine ni kumfukuza uchebe ambaye alishatengeneza team vizuri na ameipa Simba Mafanikio makubwa msimu uliopita na mpaka anaondoka Simba ilikuwa inaongoza league na team inacheza vizuri kwa miemuko ya uongozi wakamfukuza kazi badala yake wameleta kocha garasa.
NB: Mpira wa Tanzania una haribiwa na vingozi Mara nyingi kwa maamuzi mabovu wanayofanya kwa kutofuata uweredi kwenye utendaji wao.
Ni kweli, anahitaji mechi 30 zaidi ndio tutaona matunda ya ukocha wake!Sven ni kocha mzuri apewe muda, kutumia mshambuliaji mmoja ndio mpira wa kisasa huko ulaya
Sio Ulaya tu hata hapa Afrika zipo timu nyingi sana zinafanikiwa na mfumo huo. Mfumo wa mshambuliaji mmoja inahitajika uwe na mshambuliaji mnyumbulifu mwenye nguvu, uwezo wa kuhama kushoto kulia katikati muda wote wa mchezo, pumzi ya kutosha, kasi sana, akili, chenga na uwezo mkubwa wa kumiliki mpira peke yake akiwa na mabeki wawili au zaidi. Kwa Simba hatuna fowadi aliyekamilika mwenye vigezo vyote hivyo na mbaya zaidi umri umeanza kuwatupa mkono Boko na Kagere. Kwa sasa aachane na huo mfumo atumie mfumo wa washambuliaji wawili ili apunguze presha kwa viungo na mabeki wake timu ipate ushindi ichukue ubingwa ili msimu ujao yeye mwenyewe asajili wachezaji kulingana na mfumo unaoutaka yeye kama bado atakuwepo. Tujiulize mabeki na viungo wakabaji wa Simba walikuwa hawa hawa wakati ligi inaanza lakini kwa nini sasa hivi wanaonekana ni wabovu; jibu ni kuwa mwanzoni mwa ligi presha kwao ilikuwa ndogo kwa sababu timu zilibaki nyuma kuwahofia Kagere na Boko. Na timu nyingi zenye washambuliaji wakali sasa hivi zinatumia mfumo wa kukaba kwa kushambulia timu pinzani muda wote wa mchezo kwa hiyo timu pinzani inakuwa kazi yake kuokoa tu mpaka inashindwa kupangilia mashambulizi zaidi ya kutegemea "counter attack"Sven ni kocha mzuri apewe muda, kutumia mshambuliaji mmoja ndio mpira wa kisasa huko ulaya