GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 60,660
- 121,325
Nianze kwa kusema tu kwamba nimepokea kwa masikitiko makubwa sana ‘ tetesi ‘ ambazo naanza kuziamini kwamba Kocha Mkuu Mfaransa Pierre Lechantre ameondoka Simba SC kutokana na sababu ambazo kwa Mtu makini ukizisikia unaweza kukubali kwamba Wazungu wanapotudharau Waafrika kila uchao huwa hawakosei kwani tunastahili.
Simba SC ni Klabu pekee ambayo mpaka sasa japo imepata haya mafanikio lakini baso inaendeshwa ‘ Kiswahili / Kipuuzi ‘ sana hasa katika upande mzima wa Utendaji wake ambao binafsi kama GENTAMYCINE nimekuwa nikiupigia kelele humu Jamvini mara kwa mara na nasikitika kusema kwamba mambo bado hayajabadilika.
Uongozi wa Simba SC na hapa nawazungumzia sana sana Wajumbe wa Kamati ya Utendaji ya Simba SC ( sitowataja majina yao ila wanajijua ) ambao leo sifichi kusema kwamba Wao ndiyo wamekuwa chanzo cha matatizo ndani ya Klabu mara kwa mara hadi kufikia hatua ya kuondoa ‘ ustawi ‘ mzuri katika Kikosi na Benchi la Ufundi.
Wajumbe hawa wa Kamati ya Utendaji ya Simba SC ndiyo wamekuwa wakiongoza kwa kupiga majungu, kuwagawa Wachezaji na kubwa zaidi kumuingilia sana Kocha hasa katika upangaji wa Kikosi ili mradi tu wale Wachezaji wao waliowaleta Simba SC wacheze kisha waweze Kugawana nao ‘ Posho ‘ ( hapa namaanisha 10% ) ambazo zimezoeleka Simba SC na ndizo zinawaweka hapa mjini.
Nianze tu kwa Kukiri Kwanza kwamba huyu Kocha Masoud Djuma Irambona siyo Kocha mbaya na nimpe tu pongezi zake za kuweza kuiongoza vyema Simba SC hasa pale kulipokuwa na matatizo katika Benchi la Ufundi kipindi cha Kocha Omog.
Ila kama kuna Kocha ambaye ni ‘ Mnafiki ‘ na mpika ‘ Majungu ‘ ndani ya Simba SC basi ni huyu Kocha Masoud Djuma Irambona. Binafsi kama GENTAMYCINE nina Urafiki mkubwa na mzuri tu na baadhi ya Wachezaji ‘ waandamizi ‘ wa Simba SC na hata Kiongozi mmoja Mkuu wake na mara kwa mara nimekuwa nikipata taarifa kwamba Kocha Masoud Djuma ‘ hapendezwi ‘ Yeye kuwa Kaimu Kocha Simba SC kwa Kigezo kwamba anajiona ‘ anatosha ‘ kuwa Kocha Mkuu.
Ni Masoud Djuma Irambona huyu huyu ambaye amekuwa na tabia za kuwagawa Wachezaji fulani fulani wa Simba SC na kuwajaza ‘ majungu ‘ ili wacheze chini ya Kiwango kisha Kocha Mkuu aonekane hafai ili akifukuzwa basi Yeye awe Kocha Mkuu. Na tatizo hili la Masoud Djuma hajalianza tu kwa Kocha Lechantre bali alilianza tokea alipokuwepo Kocha Joseph Maurice Omog huku akishirikina kwa karibu sana na Wajumbe wawili wa Kamati ya Utendaji ( majina nayahifadhi ila kuna mmoja wapo hapo ana tabia na vitendo ambavyo huwa vinaashiria ni Shoga mzuri tu na naamini Wana Simba SC na Watu wa mpira mnamjua vizuri sana tu )
Huyu Kocha Masoud Djuma Irambona asichokijua tu ni kwamba hakuna mahala ambapo kuna Watu ‘ Wanafiki ‘ kama ndani ya Klabu ya Simba na kwamba hao ambao leo hii wanamjaza ‘ Ujinga / Upepo ‘ ili tu watimize malengo yao ipo Siku hao hao ndiyo watakaompigia ‘ zengwe ‘ kubwa ili afukuzwe / afurumushwe kwani hii ‘ dhambi ‘ hawajaianza leo.
Tabia hii ya ‘ Unafiki ‘ aliyonayo sasa Masoud Djuma Irambona alikuwa nayo Kocha msaidizi aliyeondoka Mganda Jackson Mayanja a.k.a Mia Mia na nakumbuka ni Mimi huyu huyu GENTAMYCINE niliwahi kuandika humu nikimjibu Mtu kwamba ‘ dhambi ‘ anayoitengeneza Mayanja ndani ya Kikosi cha Simba SC ipo siku itamtokea puani na kweli ilikuja kutokea vile vile ambapo alikuja kuachwa Simba SC katika hali ya aibu sana na sasa analima zake tu Ndizi huko Uganda Kwao.
Kinachonisikitisha hasa Mimi GENTAMYCINE ni kwamba Wapenzi na Mashabiki wengi wa Simba SC uelewa Wao wa masuala ya mpira ni mdogo sana lakini ndiyo hao hao ukienda katika ‘ Vibanda Umiza ‘ utawakuta wamekodoa macho yao wanatizama mipira ya Ulaya lakini bado hawabadiliki tu.
Mtu anayejua mpira vizuri kabisa hawezi kusema kwamba Simba SC haichezi mpira mzuri na wa kuvutia. Hivi kinachotakiwa ni matokeo au mchezo mzuri? Hivi Manchester United wanacheza mpira mzuri? Je wanafanya vibaya? Kama Kigezo ni Timu kucheza mpira mzuri na wa kuvutia kwanini hadi leo Arsenal FC inaucheza huo mpira lakini haina mafanikio yoyote ndani ya miaka 20?
Haingii akilini leo hii unamsikia Mshabiki / Mpenzi wa Simba SC mishipa ya shingo na macho yakimtumbuka kabisa akisema kwamba Timu akabidhiwe Kocha Msaidizi Masoud Djuma Irambona kwamba Timu haichezi vizuri huku hapo hapo wakisahau kwamba ni Kocha huyu huyu Pierre Lechantre ndiyo amesaidia kutufanya hadi tuwe Mabingwa na huyo Masoud akiwa tu anamsaidia kwa mambo machache.
Katika michuano ya SportPesa Super Cup huko Nakuru nchini Kenya baada ya Simba SC kutoka Sare na Timu ya Kariaobangi na kupita kwa mikwaju ya Penati Mashabiki / Wapenzi ‘ Wapuuzi ‘ wa Simba SC walidai Kocha Lechantre afukuzwe kwakuwa tulipita kibahati. Ni jana tu Simba SC ambayo ilikuwa chini ya ‘ Mnafiki ‘ Masoud Djuma Irambona nayo imefuzu kwa muundo ule ule je mbona hadi leo hatusikii kwamba Kocha Masoud nae afukuzwe?
Ni dhahiri kabisa kwa Kocha ambaye hadi amezifundisha Timu nyingi na kubwa za Taifa hasa katika Bara la Afrika ikiwemo The Indomitable Lions Cameroon lazima tu atakuwa ni ‘ Mweledi ‘ na anayeamini ‘ Falsafa ‘ zake na ni lazima tu Makocha kama hawa wakikutana na Viongozi ‘ Wahuni ‘ na wa ‘ hovyo hovyo ‘ amba wengi Wao wanapatikana Tanzania hawataweza kuelewana.
Pierre Lechantre anapenda nidhamu tena ile ya hali ya juu kabisa lakini kubwa zaidi huyu Kocha hapedi kupangiwa Kikosi chake kwani anaamini kwamba kwakuwa Yeye muda mwingi anakaa na hawa Wachezaji basi anawajua vilivyo kuliko Mtu mwingine yoyote hivyo maamuzi yake yaheshimiwe.
Nimemfuatilia huyu Kocha Lechantre na mpaka leo sijaona Kosa lake halafu sijaona sababu yoyote ile ya msingi ya Simba SC kumuacha au Mashabiki / Wapenzi ‘ Wapuuzi ‘ kumpiga majungu kila uchao sana sana naona tunarudi tena nyuma hatua 50 baada ya kujitahidi kusogea kwa hatua 5 tu mbele.
Uongozi ufanye Kazi zake za Kiutawala na mambo ya Kiufundi wawaachie Benchi la Ufundi na Wao wawape tu malengo yao na wasipoyatimiza basi wanaweza wakawafukuza. Siamini kama makubaliano ya Simba SC na Pierre yalikuwa ni Simba SC icheze mpira mzuri bali naamini yalikuwa ni kwamba aifanikishe Simba SC kuchukua Ubingwa wa VPL ambao tuliusotea kwa miaka mitano ( 5 )
Ikumbukwe hata pale ukiwa unafanya Mapenzi na Mkeo katika kutafuta Mtoto dhumuni kubwa huwa haliwi unavyokata Viuno vyako vya KwasaKwasa na Ndombolo ya Solo bali kinachoangaliwa sana ni uwezo wako wa ' Kumkojolea ' vizuri Mbegu zako za Kiume ili ziweze Kushika Mimba na akuzalie Mtoto ambaye ndiyo hitaji lako.
ANGALIZO
Wale ambao mmekuwa na tabia za kuchukua 'Chambuzi ' zangu za humu JamiiForums na kujifanya ni zenu tafadhali heshimuni Taaluma za Watu na nawaombeni kama mkitumia hii ' analysis ' yangu au haya ' maudhui ' yangu basi nipeni haki yangu ya kufanya Credit / Acknowledgement Kwangu ili mnitie moyo na acheni kufanya hila kwani hata Mimi naumiza sana Kichwa hadi nakuja na Kitu kama hiki.
Nawasilisha.
DALILI ZA MATATIZO SIMBA SC

UNAFIKI WA KOCHA MASOUD DJUMA IRAMBONA

ASICHOKIJUA KOCHA MASOUD DJUMA IRAMBONA
Huyu Kocha Masoud Djuma Irambona asichokijua tu ni kwamba hakuna mahala ambapo kuna Watu ‘ Wanafiki ‘ kama ndani ya Klabu ya Simba na kwamba hao ambao leo hii wanamjaza ‘ Ujinga / Upepo ‘ ili tu watimize malengo yao ipo Siku hao hao ndiyo watakaompigia ‘ zengwe ‘ kubwa ili afukuzwe / afurumushwe kwani hii ‘ dhambi ‘ hawajaianza leo.
Tabia hii ya ‘ Unafiki ‘ aliyonayo sasa Masoud Djuma Irambona alikuwa nayo Kocha msaidizi aliyeondoka Mganda Jackson Mayanja a.k.a Mia Mia na nakumbuka ni Mimi huyu huyu GENTAMYCINE niliwahi kuandika humu nikimjibu Mtu kwamba ‘ dhambi ‘ anayoitengeneza Mayanja ndani ya Kikosi cha Simba SC ipo siku itamtokea puani na kweli ilikuja kutokea vile vile ambapo alikuja kuachwa Simba SC katika hali ya aibu sana na sasa analima zake tu Ndizi huko Uganda Kwao.
UPUUZI WA MASHABIKI / WAPENZI WA SIMBA SC
Kinachonisikitisha hasa Mimi GENTAMYCINE ni kwamba Wapenzi na Mashabiki wengi wa Simba SC uelewa Wao wa masuala ya mpira ni mdogo sana lakini ndiyo hao hao ukienda katika ‘ Vibanda Umiza ‘ utawakuta wamekodoa macho yao wanatizama mipira ya Ulaya lakini bado hawabadiliki tu.
Mtu anayejua mpira vizuri kabisa hawezi kusema kwamba Simba SC haichezi mpira mzuri na wa kuvutia. Hivi kinachotakiwa ni matokeo au mchezo mzuri? Hivi Manchester United wanacheza mpira mzuri? Je wanafanya vibaya? Kama Kigezo ni Timu kucheza mpira mzuri na wa kuvutia kwanini hadi leo Arsenal FC inaucheza huo mpira lakini haina mafanikio yoyote ndani ya miaka 20?
Haingii akilini leo hii unamsikia Mshabiki / Mpenzi wa Simba SC mishipa ya shingo na macho yakimtumbuka kabisa akisema kwamba Timu akabidhiwe Kocha Msaidizi Masoud Djuma Irambona kwamba Timu haichezi vizuri huku hapo hapo wakisahau kwamba ni Kocha huyu huyu Pierre Lechantre ndiyo amesaidia kutufanya hadi tuwe Mabingwa na huyo Masoud akiwa tu anamsaidia kwa mambo machache.
Katika michuano ya SportPesa Super Cup huko Nakuru nchini Kenya baada ya Simba SC kutoka Sare na Timu ya Kariaobangi na kupita kwa mikwaju ya Penati Mashabiki / Wapenzi ‘ Wapuuzi ‘ wa Simba SC walidai Kocha Lechantre afukuzwe kwakuwa tulipita kibahati. Ni jana tu Simba SC ambayo ilikuwa chini ya ‘ Mnafiki ‘ Masoud Djuma Irambona nayo imefuzu kwa muundo ule ule je mbona hadi leo hatusikii kwamba Kocha Masoud nae afukuzwe?
UWELEDI WA KOCHA PEIRRE LECHANTRE NDIYO UNAOMUHUKUMU KIKOSINI
Ni dhahiri kabisa kwa Kocha ambaye hadi amezifundisha Timu nyingi na kubwa za Taifa hasa katika Bara la Afrika ikiwemo The Indomitable Lions Cameroon lazima tu atakuwa ni ‘ Mweledi ‘ na anayeamini ‘ Falsafa ‘ zake na ni lazima tu Makocha kama hawa wakikutana na Viongozi ‘ Wahuni ‘ na wa ‘ hovyo hovyo ‘ amba wengi Wao wanapatikana Tanzania hawataweza kuelewana.
Pierre Lechantre anapenda nidhamu tena ile ya hali ya juu kabisa lakini kubwa zaidi huyu Kocha hapedi kupangiwa Kikosi chake kwani anaamini kwamba kwakuwa Yeye muda mwingi anakaa na hawa Wachezaji basi anawajua vilivyo kuliko Mtu mwingine yoyote hivyo maamuzi yake yaheshimiwe.
Nimemfuatilia huyu Kocha Lechantre na mpaka leo sijaona Kosa lake halafu sijaona sababu yoyote ile ya msingi ya Simba SC kumuacha au Mashabiki / Wapenzi ‘ Wapuuzi ‘ kumpiga majungu kila uchao sana sana naona tunarudi tena nyuma hatua 50 baada ya kujitahidi kusogea kwa hatua 5 tu mbele.
NINI KIFANYIKE?