Simba SC Uwezekano wa Kutolewa upo

Megalodon

JF-Expert Member
Joined
Apr 9, 2021
Posts
3,534
Reaction score
7,866
Mpira huwa na matokeo ya KIKATILI sana. Nadhani wadau wa soka tujiandae kisaikolojia, maisha sio marahisi kama jinsi tunavyowaza.

Tujiulize Simba ilifika je hapa kwenye michuano hii. Tulifanyiwa Surprise moja ya ajabu pale LUPASO, hakuna aliyeamini.

Hiyo team yenyewe tunajua ilipo now? Galaxy inashika mkia kwenye kundi lake na ni lazima itoke. Hii ni ishara kwamba simba inakuzwa na kelele na ma promotion yasiyo na tija, reality on the ground ni tofauti kabisa.

Asec inakikosi kizuri, mchezaji mwenye umri mkubwa pale ni miaka 22 , wapo energetic , young and smart, kile kikosi next FY kitakuwa ni moto.

Simba Ina changamoto nyingi, kuanzia kocha , kocha pablo hana psychological tags za kufundisha Africa, hilo ni tatizo moja wapo, Tatizo lingine ni Simba kuamini katika ujinga, huwezi kuwa timu ya ushindani na striker kama Kagere , au Mugalu , ni kupoteza muda.

Hakuna mpira wa inshallah inshallah, mpira ni Investment. Uki invest Vyema , likelihood ya kufika mbali ni kubwa.

Naishauri Simba ifanye usajili wenye tija na kuacha fantasy za mitandao au ushindani wa kugombea wachezaji na Yanga , ni ujinga.

Nendeni west Africa huko Burkinafaso, Ghana, Ivory’s Cost , Cameroon , kuna vitoto vipo safi na wana miili mizuri na wana Nature za kimpira.... acheni kukomaa na watu wazeee , mnatoa expectation kubwa kwa mashabiki halafu uhalisia ni kubahatisha.

Hata ile timu ya Morocco , hamkuifunga, ukweli ni kwamba Mlifungwa But fitna ilitawala.

Kufungwa na Asec Goli 3 na Penati 2 , huo ndio uwezo wenu, vile vitoto vingi ni under 20 vina spirit na ndoto za ku Excel soka lao la kulipwa huko ulaya.

Yaani hata Simba ikifika Robo fainali, asilimia 95% , hapo ndio itakuwa ni mwisho wao. Hakuna kikosi cha kucheza nusu fainali.

Pamoja na yote , Simba ana asilimia 55 ya kwenda mbele. Asec ana asilimia 50 ya kwenda mbele , BERKANE Ana asilimia 55 ya kwenda mbele, GENDERMARIE ana asilimia 15 ya kwenda mbele , pamoja na uchache wake, ni wazi wanaweza kumbania Mnyama asipite, yaani any suluhu, Simba Out.
 
kundi la utopolo ,azam na somalia u-23 mchuano ni mgumu sana ,azam fc anaongoza kundi baada ya kumpiga somalia u-23 goals 3 ila sare ya uto na wasomali imewaweka pazuri, utopwinyo wanawakilisha nchi vizuri sana kimataifa
 
Gendarmerie ili wapite ni lazima wao washinde halafu Berkane afungwe kitu ambacho ni kigumu.

Kwa kikosi chetu ilifika muda nikasema kumbe ni afadhali tuliangukia shirikisho. Champions league tungepata shida zaidi.

Kufungwa na Galaxy kulichangiwa na mengi, pia wale watoto ni kama ilikuwa fruk tu.

Halafu ukitaka kuzungumza kuhusu kuzifunga team kwa mkapa, Sio Berkane tu team yeyote ile kwa mkapa ni kijitahidi huwa ni sare. mara chache sana hutokea kama yale ya Galaxy Ndio mpira wa afrika ulivyo.

Mnawasifu Asec vip matokeo ya hapa mbona hamkuwazungumzia. Ni kawaida wachambuzi wetu nyie kuzodoa team inapokuwa imefanya vibaya. Ikifanya vizuri hamhangalii au kutafuta hayo mapungufu ili hali huwa yanakuwepo.

Binafsi match na Berkane tulishinda ila sikufurahi kwa nafasi nyingi tulizokosa. Hata maneno yalikuwa mengi ni vile game ilisha 1-0, ingekuwa 3-0 au 4-1 hakuna angezungumzia fitna. Ila ilikuwa moja 1-0 na ukiangalia goal lilikataliwa, penalty etc.
 
Gendarmerie ili wapite ni lazima wao washinde halafu Berkane afungwe kitu ambacho ni kigumu.

Kwa kikosi chetu ilifika muda nikasema kumbe ni afadhali tuliangukia shirikisho. Champions league tungepata shida zaidi.
...

Ukweli kwenye fair play , île game na waarabu tulizingua. Sidhan kama ni neno sahihi kusema tulizingua bali ndio uwezo wetu wa chini pia wachezaji hawana Strength .

Ni kwanin mpaka ufungwe ndio ucheze vema . Simba inahitaji wachezaji wenye mental strength ; binafsi ninawakubali sana west Africa Kwenye mpira... they are good

Tukubali simba bado hatuna consistency.... yaani mwaka huu tunacheza Robo fainali klabu bingwa, next season , tunatolewa Kwenye Preliminary, next year tunaishia shirikisho..... hiyo ni ishara kwamba hatujawa na kikosi madhubuti na chenye tija.

Promotion ni nyingi kuliko investment
 
Mkuu hujawahi kosea Simba ni Mkolo tu na Mpira hawana.. habari ya mjini now ni Yanga tu💪
 
Kwavile wanategemea tuvitu vitu ili kushinda kwa Mkapa basi bila shaka watashinda. Mechi ambayo wanakuwa na uhakika wa matokeo huwa wanadharau kufanya mipango na mikakati yao kwavile wanajua moinzani wake ni wepesi wameshamaliza shuguli wakiwa away nyumbani kufa ni lazima.

Hapa utaona kwenye mechi dhidi ya UD Songo walivyoenda kutoa sare ya bils bila basi hawakuwekea kwenye mbinu na mipango yao wakajiamini wakatolewa.

Mechi dhidi ya galaxy hivyo hivyo wakaenda away wakapata advantage ya magoli mawili wakaona hawa wepesi haina haja kutumia nguvu nyingi marudiano, tunawaweza kuwafunga kwa uwezo wa timu yety kilichotokea hapa ni balaa.

Hivyo kwavile ni mechi ambayo inauwaumiza vichwa ili kufuzu basi itafanyika kila mbinu na slogan itatungwa kama kawaida na mwisho itapata ushindi
 
Gendarmerie ili wapite ni lazima wao washinde halafu Berkane afungwe kitu ambacho ni kigumu.

Kwa kikosi chetu ilifika muda nikasema kumbe ni afadhali tuliangukia shirikisho. Champions league tungepata shida zaidi..

Unadhani Gendarmerie watakuwa na mentality hiyo? Wao watakuwa na akili ya kutafuta alama tatu ili baada ya dakika 90 ndipo wajue nini kimetokea kwenye mechi ya Berkane..

Mechi ya Simba vs Assec kwa Mkapa, pamoja na simba kuongoza goli moja lakini Assec walionekana na utulivu mkubwa mno yaani ukiangalia uchezaji wao na Simba unaona ni mbingu na ardhi yaani wana kila kitu.

Ilipotokea wamesawazisha lile goli ndio kabisa wakaendalea kuu win mchezo hadi pale ambapo kipa wao kafanya kosa ambalo hata kipa wa ndondo hawezi kufanya kosa lile, jambo ambalo likawatoa mchezoni. Ni tuko lililotokea kutokana na mazingira ya Simba wanapotumia uwanja wa mkapa
 
Simba inasumbuliwa na wachezaji kutokujituma uwanjani. Ni wavivu na wazembe. Cha ajabu kocha yupo uwanjani hapo hapo na hajui anachofanya. Vilevile kocha anachelewa kufanya sub. Kibu D anaharibu mpira kutoka dkk ya kwanza na kufanyiwa sub dkk ya 70.
 
Kipa wa Asec ana 36years. Futa kauli
 
Kipa wa Asec ana 36years. Futa kauli
Kuna wachezaj Kam watatu ni watu wazima kabsa pale afu yey anazan kumpta mchezaj wa miaka 18 au 19 Kwa nchi za west Africa ni kitu kidgo umri huo weng wanatolewa macho na vilabu vya ulaya yule dogo aliyekosa penati ya Kwanza ana miaka 17 tayari anatakiwa na vilabu vya ulaya
 
Waligombania penalty ili kupalilia CV za kuendea ulaya. Manula akawaambia msigombanie,wote mtapiga.
 
Ila bongo bwana team isifungwe yaani kila siku team ishinde hakuna team ya hvyo duniani hata kama ni kweli kuna mapungufu ila sio kwa hoja hizo juzi real Madrid kafa 4 mtungi hakuna aliyetegemea na ilikuwa wafe nane wale ingekuwa bongo kocha angefukuzwa wachezaji wangetukanwa yaani kiufupi mpira sisi bado yaani nje ya uwanja na ndani ya uwanja.
 
ajabu sana Asec walifungwa hapa hakuna aliyeongea na kuwasifu au hata kuwatizama tu kwa jicho watu wakakausha. Leo nao wameshinda kwao watu eti ndio wanawaona bora na kuuona ubovu wa simba. Hii ndio bongo.
 
ajabu sana Asec walifungwa hapa hakuna aliyeongea na kuwasifu au hata kuwatizama tu kwa jicho watu wakakausha. Leo nao wameshinda kwao watu eti ndio wanawaona bora na kuuona ubovu wa simba. Hii ndio bongo.
Ilipofungwa na simba walisema asec ni team mbovu ni academy kama azam Leo wamegeuka ila utopolo kwa kujitoa ufahamu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…