Simba Sc wamemrejesha Clatous Chama kuokoa Jahazi

DuaZaMama

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2025
Posts
1,882
Reaction score
4,153
Klabu ya Simba SC imemrejesha rasmi kiungo wake wa zamani, Clatous Chama, akitokea klabu ya Singida Black Stars. Hii ni mara ya tatu kwa Chama kujiunga na wekundu wa Msimbazi, baada ya awali kuwasili kwa mara ya kwanza akitokea Lusaka Dynamos FC ya Zambia, kisha kusajiliwa tena akitokea RS Berkane ya Morocco kabla ya kwenda Singida Black Stars.

Chama ametambulishwa rasmi na uongozi wa Simba SC na tayari ameungana na kikosi cha timu hiyo kilichosafiri kuelekea Tunisia alfajiri ya leo, Januari 21, 2026, kwa ajili ya maandalizi ya mechi zijazo za kimataifa.

Pia Soma: Tetesi: - Clatous Chama kurejea Simba Sc kwa mara ya 3
​
 
Kwa aina hii ya usajili, simba isahau kuchukua ubingwa wowote ule ndani na nje ya nchi!

Kwa sababu zama za Clotus Chama zilishapita long time kitambo. Na hata sasa jamaa anachezea jina tu. Ila kiwango chake siyo kile cha miaka kadhaa iliyopita alipoitumikia timu ya simba.
 
Hivi Valentino Nouma alikuwa na shida ipi?
Mbona Simba haitulii na watu?
Sasa Kibabage anaenda kubabaga nini pale....
Hata Inonga ilitakiwa abakishwe tangu......anyway tuachana na hayo.

Wakati mwingine sio mbaya hata kumpunguzia nguvu mpinzani wako mkuu kama ambavyo yeye anavyokufanyia kila anapojisikia
Kama Yanga iliwasajiri
Chama, zimbwe, Israel, Mkude, okra
Kwanini Simba isimsajiri boka, naona kama kapoteza furaha pale
 
Hii ni dalili kwamba the club is unmoney🤣
 
Wamtafute na John Bocco akwasaidie
 
Hapo ni wazi kwamba kuna watu wanapiga hela kwenye sajili hizi. Huo ndio ukweli kwani watanzania ni watu wenye hulka ya ufisadi hadi watawala.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…