Simba SC wameshindwa kuwafunga Watoto

ukiingia vitani na silaha dhaifu,usimlazimishe adui yako naye atumie silaha dhaifu eti ili mlingane. Kila mtu apambane na hali yake. Hakuna ushauri wowote mzuri utakaotoka kwa adui kuhusu matumizi ya silaha. Simba imesonga mbele kwa gap la points mbili, Yanga imesonga mbele kwa gap la goal difference. hapo ndipo ilipo tofauti. Na kama vile haitoshi, Simba haijaruhusu goli lolote wakati Yanga imeruhusu magoli mawili. Kila mtu apambane kivyake, tuache uoga
 
Nyani haoni kundule. Nyie Utopolo mmeishinda KMKM? Au unaropoka bila kushirikisha medulla oblongata yako
Yanga hakupania game na ndio maana hata line up ilikua sio ile yenyewe...mbali na hapo yanga imetikisa nyavu zao mara 2...yanga kapambana na timu inayo ongoza ligi znz....simba kamili imepambana na timu ya pili kutoka mwisho ktk msimamo wa ligi znz....kwa maana kwamba ktk msimamo baada ya mlandege inafuata zimamoto ndio kishika mkia.....
Jitafakarini acheni matusi...mpo hatarini!
 
Hadhi, umaarufu na hata ubora wake uko palepale. Hakuna mchezaji Simba anamzidi Feitoto kwa yote hayo currently
Wa kawaida sana huyo ila mnamuona anajua kwa vile yupo kwenye klabu isiyo na malengo makubwa.Mchezaji bora uthibitisha ubora wake kwenye mechi kubwa. Dhidi ya rivers utd au kule Afcon alikuwa anaruka ruka tu.
 
Wewe ni kabwili fc
 
Tuletee na Rivers ilikuwa ya ngapi usikimbie[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]
 
Mpira wa Tanzania ni wa aina yake kwa kweli
Huko ulaya man u anafungwa na team ina buruza mkia ,
Real Madrid naye hivyo hvyo ila bongo sasa simba na yanga zisifungwe hiyo itakuwa mada week nzima.
 
Matokeo ya kikatili kwenye mpira wa miguu ni kitu cha kawaida sana. Lakini Simba kupata sare kwa Mlandege ilisababishwa na wao wenyewe kwa sababu zifuatazo:-

1. Wachezaji wa Simba kuidharau Mlandege toka mwanzoni mwa mchezo na kadiri muda ulivyokuwa unaenda iliwapa sana moyo Mlandege wakakza zaidi..
2. Simba kukosa namba tisa aliyekamilika kwani waliopo Simba sasa wote miili migumu hakuna anayenyumbulika. Na hili la kutafuta namba tisa ya magoli wakilidharau basi watapata sana shida kuutetea ubingwa wao na pia itawawia vigumu kufanya vizuri kwenye Shirikisho Afrika. Sio lazima watafute mchezaji huyo kutoka nje kwenye dirisha hili wanaweza hata kumchukua Lusajo wa Namungo kuwa "back up" Kagere, Mugalu na Boko kwa kipindi hiki cha mpito.
3. Mlandege walipaki basi toka mwanzo na Simba walikosa "plan B" ya kuvunja mtego wao. Ile mechi ingechezwa hata mpaka saa sita usiku bado Simba wasingefanikiwa kupata hata bao moja kwa sababu waliendelea kucheza kwa namna ile ile toka mwanzo huku wakitegemea wapate ushindi.
4.Wakati wa kushambulia mawinga na viungo wa Simba walikuwa wanamuacha Mugalu peke yake kiasi mipira mingi iliyokuwa inadondoka baada ya Mugalu kupambana ilikuwa inaokolewa kirahisi na wachezaji wa Mlandege.
5. Wachezaji wengi wa Simba hasa mawinga na washambuliaji wameanza kucheza na jukwaa na kuwa wabinafsi badala ya kucheza kitimu kila mmoja anataka akae muda mrefu, akokote mpira kwa mbali mrefu, apige chenga au afunge mwenyewe ili asifiwe na mashabiki jukwaani. Inabidi waelezwe mapema waache hiyo tabia warudi wacheze "team work" kama zamani.
6.Ili timu moja ipate ushindi uwanjani ni lazima mpinzani afanye makosa aidha yeye mwenyewe au alazimishwe na mpinzani wake kufanya makosa. La kwanza la kufanya makosa Mlandege walikuwa makini hawakufanya makosa wenyewe hata kama yalikuwepo ni madogo sana na kwa hili hauwezi kuwalaumu Simba. Lakini la pili la kumlazimisha mpinzani wako afanye makosa lilikuwa ndani ya uwezo wa Simba lakini walishindwa kulitimiza. Simba walipaswa wawe na wachezaji wawili mpaka wa tatu karibu na boksi la Mlandege wakarti wanashambulia lakini mara nyingi alikuwa Mugalu peke yake kiasi ikawa rahisi sana kwa mabeki wa Mlandege kumficha. Lakini kibaya zaidi hata pale Mlandege walipokuwa wanaenda kushambulia lango la Simba na wachezaji wa Simba wakipata mpira bado walikuwa wanacheza "square pass" upande wao na hivyo kuwapa muda Mlandege kurudi kwa wakati na kujipanga kuzuia. Inabidi benchi la ufundi la Simba na wachezaji wao warudi wakaangalie lile goli la pili la Simba dhidi ya Azam pasi ya Kibu halafu wafanyie mazoezi.
7. Simba kukosa mchezaji maalum mwenye utaalamu wa kupiga mipira iliyokufa karibu na lango la wapinzani wakati ikitumiwa vizuri inaweza kuwa ndio njia ya haraka ya kupata matokeo. Kwa hili benchi la ufundi linapaswa kulaumiwa kwa sababu lilitakiwa limgundue mchezaji/wachezaji wenye uwezo wa kupiga mipira iliyokufa kwa usahihi kisha liwape mbinu na mazoezi zaidi ili kuwaongezea ujuzi. Lakini sasa hivi kila ikitokea faulu utaona kila mchezaji wa Simba anataka kwenda kupiga halafu wote wanapiga hovyo. Inatakiwa kabisa ijulikane nani anapiga faulu za upande wa kushoto mwa goli au nani anapiga faulu za upande wa kulia wa goli au za katikati ya goli. Kwenye baadhi ya timu unaweza kukuta ni mchezaji huyo huyo ameandaliwa kupiga faulu zote bado sio shida kikubwa tu awe ni mchezaji aliyetayaarishwa kiufundi na benchi la ufundi. Na hili pia liwe kwenye penati kwani kwa sasa Simba ndio janga lao kubwa la kukosa penati

Mwisho kwa msisitizo kabisa kamati ya usajili ya Simba, viongozi na benchi la ufundi fanyeni tathmini ya kina mtagundua kwa sasa Simba pamoja na matatizo mengi madogo madogo ya kiufundi lakini tatizo baya na kubwa na ambalo litawagharimu pa kubwa kwenye mashindano yote yajayo ni kukosekana namba tisa mwenye uwezo mkubwa wa kuipangua ngome ya timu pinzani, aweze kufunga iwe kwa kichwa, miguu, n.k. Kwa ujumla mshambuliaji mwenye uwezo binafsi wa kubadilisha matokeo hata ikitokea timu nzima imebanwa. Kwa hili ikiwezekana fanyeni maamuzi magumu ya kuachana na mshambuliaji mmoja wa kigeni halafu tafuteni mwingine mwenye uwezo zaidi hao waliopo itawasaidia.

Ni mtizamo tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…