Simba SC wanakwama Hapa 2018-2019

Simba SC wanakwama Hapa 2018-2019

mangonjoli

Senior Member
Joined
Aug 29, 2012
Posts
154
Reaction score
110
Wadau wa Soka nimeangalia klabu ya Simba msimu huu nimekutana na Mapungufu ambayo yasipofanyiwa Kazi Jahazi litazama. Hapa nimejaribu kuelezea mambo saba ambayo yanaweza yakaleta maafa msimu huu.

1. Ni muda mrefu tokea Atimuliwe kocha msaidizi masoud Juma mpaka leo kocha mkuu Patrick Aussems hajatafutiwa msaidizi hili ni kosa kubwa kwa klabu kama Simba ambayo juzi tu Imeingia katika mfumo mpya wa Kisasa.

2. Tatizo lisiloisha la kipa Aishi Manula la Kufungwa Magoli ya Faulo na mashuti ya mbali asipobadilika litaigharimu sana Timu. Nakumbuka nilishawahi kumkumbusha katika page yake ya Instagram muda sana na hakuna Mabadiliko.

3. Timu kubwa kama Simba mpaka leo haina mtaalam wa kupiga Faulo au kona . wana kona zao fupi fupi ambazo hazijawahi kuwasaidia na bado wanazitumia Kiufupi Simba hata wapate faulo 50 kwenye mechi moja usitegemee maajabu. Wakati timu kubwa kama Nkana , Al Ahly , Zamalekh , Enyimba N.k wasipokuadhibu kwa Faulo watakumaliza kwa kona.

4. Simba kabla ya kufungwa Dirisha dogo walipaswa kusajili mshambuliaji mwengine wa Kimataifa atakayemsaidia John boko maana ameanza kupoteza umakini na Goli. Boko wa sasa inabidi apoteze nafasi Tatu za wazi ndio aje afunge moja . Au angalau wampe nafasi Adam Salamba baada ya kumchezesha Boko kwa dakika zote 90. Sina uhakika lakini naamini Wachezaji wanaopaswa kuongezwa ligi ya Mabingwa kama Simba watafuzu makundi iwe klabu bingwa au kombe la Shirikisho anapaswa kuwa na leseni ya Ligi kuu Tanzania ambapo Dirisha lishafungwa.

5. Mechi za Viporo Simba zitawasumbua sana. Ni kawaida Simba huwa wanashindwa kucheza mechi za Pressure kwa hili wajipange kwelikweli. Yanga akiambiwa kuna mechi Saba za Ubingwa atashinda zote hata kwa mbinde. Lakini Simba mpe mechi tatu za Ubingwa lazima moja ataharibu.

6. Simba wana tabia za kuridhika wakishapata goli mbili wanaanza Showgame na pasi ambazo hazina Tija kwa timu mwishoe wanazidiwa na kufanya mashabiki kuwa roho juu. Rejea mechi za msimu huu za African lyon, JKT Ruvu na ya juzi dhidi KMC.

7. Simba ndio timu inayotengeneza nafasi nyingi lakini magoli ni haba. Katika nafasi Tano wanaweza kupata moja. Wakati kiuhakika inatakiwa katika nafasi mbili upate moja au unaingia wavuni zote mbili . Hii ni vita!!
 
Hujaambiwa Suala la ukocha . Nimejaribu kuangalia maeneo ambayo Timu inaweza kukwama. Kama unaweza kunipinga kwa hoja karibu.
Mchezo wa soka huwa hauna timu timamu siku zote.

Ndiyo maana timu inafungwa na mara nyingine kutoa draw. Kwanini unadhani matatizo ya Simba ni makubwa kuliko ya Lipuli?
 
Maneno KUNTU tena kwa uyo manula ndio umenena, hana lolote alaf anafungwa magoli ya kishamba sana, mfano magoli ya nkana ya hovyo
 
Maneno KUNTU tena kwa uyo manula ndio umenena, hana lolote alaf anafungwa magoli ya kishamba sana, mfano magoli ya nkana ya hovyo
Ndio maana Manula mpaka Leo nimeshindwa kumuita Tanzania One. Bado hajaweza kuvaa viatu vya Mwameja, Nemes , kaseja , Iddi pazi , Ivo Mapunda na wengineo . Tanzanis One gani unafungwa magoli ya Aina moja.
 
... 2. Tatizo lisiloisha la kipa Aishi Manula la Kufungwa Magoli ya Faulo na mashuti ya mbali asipobadilika litaigharimu sana Timu. Nakumbuka nilishawahi kumkumbusha katika page yake ya Instagram muda sana na hakuna Mabadiliko.
Ndio maana Manula mpaka Leo nimeshindwa kumuita Tanzania One. Bado hajaweza kuvaa viatu vya Mwameja, Nemes , kaseja , Iddi pazi , Ivo Mapunda na wengineo . Tanzanis One gani unafungwa magoli ya Aina moja.
Hii ya Manula naona sasa watu wanakaririshana, na imekuwa wimbo. Mbona magoli aliyoruhusu ni machache ukilinganisha na hatari alizookoa? Yaani unaona ni bora golikipa anayefungwa magoli 10 ndani ya eneo la kumi na nane kuliko Manula anayefungwa magoli matano nje ya eneo la kumi na nane, kwa idadi hiyo hiyo ya mechi? Kwa nini hatuzingatii hatari alizookoa ambazo kipa mzembe angefungwa? Tuache kukariri, eti tumuache Manula kwa kuwa anafungwa magoli ya staili moja, tumsajili Kindoki eti kwa kuwa anafungwa magoli ya staili tofauti tofauti
 
Kwa hiyo asajiliwe Mwameja, Pazi, Kaseja na Ivo Mapunda? Kwa sasa Manula ndio Tanzania One
 
Hujaambiwa Suala la ukocha . Nimejaribu kuangalia maeneo ambayo Timu inaweza kukwama. Kama unaweza kunipinga kwa hoja karibu.
Hakuna ulichoongea cha uongo hapo, ni ukweli mtupu. Kuna medhi wamepoteza points 3 kizembe kabisa kama mechi yao na Yanga, Lipuli na Mbao.

Simba hawana kasi ya kuwachanganya mabeki, afadhali kikosi kilichocheza na KMC kilikuwa ba pace mpaka mabeki wanachachawa
 
H
Hii ya Manula naona sasa watu wanakaririshana, na imekuwa wimbo. Mbona magoli aliyoruhusu ni machache ukilinganisha na hatari alizookoa? Yaani unaona ni bora golikipa anayefungwa magoli 10 ndani ya eneo la kumi na nane kuliko Manula anayefungwa magoli matano nje ya eneo la kumi na nane, kwa idadi hiyo hiyo ya mechi? Kwa nini hatuzingatii hatari alizookoa ambazo kipa mzembe angefungwa? Tuache kukariri, eti tumuache Manula kwa kuwa anafungwa magoli ya staili moja, tumsajili Kindoki eti kwa kuwa anafungwa magoli ya staili tofauti tofauti
Hatujamuongelea Kindoki hapa
 
Umewaza vyema sana
 
Back
Top Bottom