Simba SC Wataukosa Ubingwa wa Msimu 2017/18.

Simba SC Wataukosa Ubingwa wa Msimu 2017/18.

demigod

JF-Expert Member
Joined
Jan 2, 2015
Posts
8,292
Reaction score
15,250
Wasalaam.

Tumeshuhudia mtanage mkali kati ya Vijana wa Daraja la 2 yaani mashujaa wa Kijani wakimenyana na Simba SC.

Vijana hao waliweza kuwalazimisha Simba kuweka historia ambayo haikuwahi kuwekwa hapa bongo. Bingwa mtetezi kutolewa kwenye michuano ya shirikisho kwenye hatua awali kabisa.

Wapo wengi waliosema kuwa huu mchezo unaakisi taswira nzima ya bingwa huyo mtetezi jinsi na namna alivyobahatika hata kuutwaa Ubingwa huo msimu uliopita.

nilipata nafasi ya kukaa na mtu nyeti fulani wa kikosi hiko cha mabingwa watetezi, na kuniambia kuwa Simba kwa namna inavyocheza inaonekana kuwa "wachezaji wako kwenye mgomo baridi dhidi ya Kocha wao Omog". Anyway sikutaka kulijadiri hilo kiundani.

Ila kwa namna taswira inavyojionyesha ni kwamba. Jinamizi hili la kutolewa mapema zaidi kwenye michuano hii ya FA kutaipelekea Simba kutofanya vyema kwenye mechi za ligi zijazo na hatimaye kuukosa kabisa ubingwa wa msimu huu 2017/18.
 
Kama wametolewa na wamatumbi wa hapahapa hivi hao watawaweza waarab kweli
Waarab tishio la Yanga,Simba wanaijua.Wanajua wakikutana na Simba wamekutana na wanaume.Kwa vile hujui mpira ndio maana unashangaa Simba kufungwa na timu ndogo.Watu msiojua mpira mko wengi humu
 
Back
Top Bottom