Kunguru Mjanja
JF-Expert Member
- Aug 22, 2012
- 2,046
- 3,971
Omog, aliliambia Nipashe jana kuwa wamefanyia kazi mapungufu waliyoyaona kwenye mchezo uliopita dhidi ya Mbao FC na wamejipanga kuhakikisha wanaondoka Shinyanga na pointi tatu.
"Matokeo ya mchezo uliopita tumeachana nayo kwa sasa tunaangalia kwa mapana mchezo wetu unaofuata dhidi ya Stand United,"alisema Omog.
Alisema kuwa hawatarajii kufanya makosa yatakayowafanya washindwe kupata pointi tatu muhimu kwenye mchezo huo.
"Tupo kwenye maandalizi ya mchezo unaofuata, wachezaji wameumia kwa sare tuliyoipata, hivyo sitegemei kuona tunatoka sare nyingine japo mpira ni mchezo wa dakika 90 na lolote linawezekana,"alisema Omog.
Alisema mchezo dhidi ya Mbao wachezaji wake walicheza vizuri, lakini wapinzani wao walitumia vyema nafasi mbili walizozipata na kufanikiwa kupata sare kwenye uwanja wao wa nyumbani.
"Kwa sasa akili zetu zipo kwenye mchezo wa Shinyanga, tumefanyia kazi kasoro tulizoziona na tunaenda Shinyanga kwa lengo la ushindi tu," aliongeza kusema Omog.
Nipashe