Simba SC yashinda 2-0 dhidi ya Kahraba FC kwenye Mechi ya Kirafiki

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
​

Kikosi cha Simba kilichopo Misri, katika maandalizi ya msimu mpya wa NBC Premier League na mashindano ya kimataifa, kimecheza mchezo wa kwanza wa kirafiki wa kujipima nguvu na timu ya Carabat FC, ambapo Mnyama ameshinda magoli 2-0.
Your browser is not able to display this video.

Bao la Mohamed Bajaber katika mechi ya kirafiki dhidi ya Kahraba Ismailia katika uwanja wa Suez Canal Authority.​

Kahraba Ismailia SC, inacheza Ligi Kuu ya Egypt na imeshacheza mchezo mmoja wa ligi ya Egypt dhidi ya El Gouna ambayo walifungwa pia bao 1-0.

Goli la kwanza lilifungwa kipindi cha kwanza na mchezaji Mohammed Bajaber huku goli la pili likifugwa kipindi cha pili na Jonathan Sowah.

Your browser is not able to display this video.

Jonathan Sowah akifunga bao la pili katika mechi ya kirafiki dhidi ya Kahraba Ismailia​

Wikiendi ijayo Kikosi cha Simba SC kitahamisha kambi yao kutoka Ismailia kwenda Cairo ambako watacheza michezo mingine ya kirafiki kabla ya kurejea Tanzania.

​
 
Ndugu mwandishi ungetuambia pia hiyo Kahraba ni timu ya daraja la ngapi. Natambua fika ni kipindi cha pre season.
 
Ngoja utopolo na wenyewe wajibu mapigo kwa kucheza na Kimbiji Kombaini
Utopolo siku zote hucheza na wakina kimbiji kombaini, mbagara market, n k lakini mataji anabeba na Simba inayocheza mechi za kirafiki ughaibuni anatandakwa na utopolo inayocheza na kimbiji kombaini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…