Umesema ukweli mkuu.
Tena sio wachambuzi uchwara tu,bali kuna wapenzi wa Simba wengi wanapohojiwa hawaongelei possibilities, Bali wanaongelea kufungwa tu.
Nimeamini kweli ndio maana umaskini na utajiri huambukizwa.Ulizaliwa maskini historia yako itakufanya uukubali umaskini na kuona utajiri kama wa watu wengine
tu.
Utopolo aka vyura wanaitakia mabaya Simba kila mechi.
Kumbukeni hata hii kwa Mkapa walitutabiria kufungwa goli nyingi wakiwemo wachambuzi wanaokula futari kwa gsm.Lakini baada ya ushindi wa goli moja wakabadili kauli tena.
Kama wana simba wakikumbwa na ulemavu wa kufikiri kama hawa utopolo,watawapa sababu wachezaji kucheza bila kujituma kwa kuwa wanaona sie wanasimba tumeshakubali matokeo