Simba Sports Club kuna nini kimejificha?

Simba Sports Club kuna nini kimejificha?

Richlifepaul_

Member
Joined
May 26, 2024
Posts
5
Reaction score
5
@SimbaSCTanzania

Muda huu nimekosa usingizi, kwani nalala ili iweje ikiwa baadhi ya watanzania wanamaswali mengi wasiyojua majibu yao.

Viongozi wa Simba nani kawaroga kiasi kwamba mnajijali wenyewe na kusahau majukumu yenu? Mr @moodewji na wewe ujui jukumu lako mzee au yamayoendelea yanakufurahisha? Ote ninyi ni matatizo kwa kutojua wajibu wenu.

Ukilala unaota taarifa za uongo za viongozi, unaota fujo za mtandaoni, unaota machawa wanaowasemea viongozi, unaota kesho usiyoijua ya Simba pia unaota kilichosemwa na kocha na tunajua ni kweli hii taasisi imevurugwa na wachache.

@salim_tryagain anko wewe umesahau wajibu wako au ni makusudi? Kwanini uko kimya tunahitaji ukweli. Utaamka lini ulipolala au tukupe shuka nzito uendelee kulala?

#Mangungu inasemekana huna nguvu kwenye timu sasa kazi yako nini ? Toka 2020-2024 upo sehemu unanguvu unafanya nini? Wajibu wako umetimiza? Basi sema usikae kimya wewe kazi yako umetimiza au tukuache huna nguvu hapo Simba.

Wajumbe wa Simba nyie wajibu wenu mmetimiza au mnasubiri kusema hamuachii ngazi?. Hayo mliyosema kwanini hamkuyasema kipindi kile au mnamaslai binafsi?. Mngelikuwa na weredi mngeondoka/au kusema hayo kitambo.

Ote hamjui uwajibikaji "Uongozi ni mzigo ukiona mambo si mazuri unapumzika" ila ukilazimisha tutajua nyie ni wapigaji tu. Kesho si leo isiyoisha, kesho nileo isiyoisha vyema.

Mwekezaji awezi weka hela pabovu.

Nimeandika mimi, pale nilipokosea mnisamehe bado natafakari. Niwatakie siku njema. #simba
#NguvuMoja


@richlifepaul_
 
Tatizo la Simba ni kuwa na viongozi waganga njaa, mambumbumbu na wababaishaji

RIP Hans Pope
 
Back
Top Bottom