Simba, tafadhali mtoeni Said Ndemla kwenye kifungo hiki

Fact [emoji1666]

Nadhani walitaka atoke Jonas Mkude aingie ndemla halafu waanze kusema kuwa Simba inamchukia Mkude

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Fact [emoji1666]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kagera sugar wanaweza kumlipa mshahara anaopata Simba kwa Sasa?
Kwa mchezaji mwenye malengo, mwenye kipaji, mpambanaji na anayejiamini hawezi kukaa tu benchi kwenye timu eti kwa sababu analipwa mshahara mkubwa. Kwa vyovyote vile lazima atatafuta jukwaa sahihi kwenye hizi timu za kati kama Mtibwa, kagera, Ruvu, n.k. aonyeshe uwezo wake halafu hizi timu kubwa zitamfuata kwa mshahara mkubwa zaidi ya huo wanaompa sasa. Mfano mmoja Hasani Dilunga alikuwa Yanga yakatokea yaliyotokea lakini kwa kuwa alikuwa anajiamini aliachana na Yanga na kama sikosei akaenda Ruvu na baadae akaibukia Mtibwa na sasa yupo Simba tena akiwa na kiwango cha hali ya juu. Hata Kelvin Yondani Simba walianza kumpiga benchi kiajabu ajabu lakini kwa kuwa alikuwa anajiamini aliamua kuondoka na kujiunga na Yanga ili kuokoa kipaji chake vinginevyo angeng'ang'ania mshahara tu Simba Yondani angepotea mazima katika ramani ya soka.
 
Mlipili ndo nani?
Beki wa zamani wa Toto African ya Mwanza. Beki mmoja hivi fundi, ng'ado kwa ng'ado, mbishi mbishi fulani awapo kazini uwanjani, kwa mbali ana umbo kama la George Magere Masatu na hata uchezaji wake kidogo umefanana kama wa Masatu. Beki ambaye ndiye alikuwa muhimili wa ukuta wa Simba kwenye ligi ya ndani na michezo ya kimataifa miaka michache hivi iliyopita na ili kuujua ubora wake nenda "youtube" ukaangalie Simba VS Al Masry.Kwa sasa Mlipili yupo anaozea benchi pale Simba Sport Club na hakuna anayejua sababu hasa ni nini kwani alianza Ausems kumpiga benchi na hata Sven naye hajampa nafasi kabisa kuonyesha uwezo wake.

Kwangu mimi naona ajabu kwa Tairone na Kennedy kupewa nafasi ya kucheza wakati fundi Mlipili hata benchi hakai. Inawezekana labda makocha wameona kiwango chake kimeshuka sana maana wao ndio wapo naye mazoezini kila siku. Lakini yote kwa yote ni wakati wake sasa kuondoka Simba ili aokoe kipaji chake kwani umri wake bado unamruhusu kucheza mpira kwa muda mrefu ujao na si kuendelea kukaa Simba wakati hata kwenye listi ya wachezaji wa akiba mara nyingi anakuwa hayupo.
 
Basi mtoeni kwa mkopo ili asiue kipaji na bado aendelee kuwa msaada wa timu baadae,
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Acha Majungu muda wake ukifika nae atapata tu nafasi. Mbona hamshangai jinsi Jonas Mkude alivyokaa benchi Kipindi cha akina Marehemu Mafisango ila alivumilia na kujifunza kutoka Kwake na sasa ni Mchezaji tegemeo ndani ya Simba SC?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…