Simba timu mnayo, ajirini mtaalam ama wafundisheni saikolojia wachezaji wenu mtatwaa CAF Champions League

FRESHMAN

JF-Expert Member
Joined
Sep 29, 2011
Posts
9,137
Reaction score
34,793
Habari wadau,

Mimi mwanayanga. Ila namkubali mo kwa uwekezaji wa Simba.

Natazama sana mashindano ya CAF Champions League kila msimu. Mimi ni die hard African football fan boy. Natazama CAF Champions League kuliko UEFA.

Mashindano ya CAF ni magumu sana na yana tofaut sana na UEFA, maana ni pride sana, yaani timu zinachezea pride.

Ukiwa away hata uwe na timu kali vipi, unashambuliwa kama mwizi na kama hauko vizuri kisaikolojia unafungwa nyingi.

Simba kilichobaki iwekeze kwenye saikojiaza wachezaji, ikiwezekana wawe na mtaalamu wa kuwaongoza saikolojia.

Maana simba bila saikolojia haiwez pata hata sare mjini casablanca kwenye mechi na waydad ama raja Casablanca. Simba haiwezi pata matokeo mjini aba kwenye mechi na enyimba pale Enyimba Stadium katikati ya Igboland, Aba State, (maana wenye Enyimba ni kabila kubwa Nigeria wa Igbo na uwanja wao wa nyumbani upo kijijini kwao)

Ni sawa una mechi na Wazaramo harafu mechi unaicheza msanga ama Wakurya mechi inachezwa Tarime nyamwaga) Simba haiwez pata hata sare pale mjini Pritoria kwenye Lucas Moripe Stadium kwenye mechi na Memelodi Sundown, bila saikolojia siioni Smba ikipata hata sare pale mjini Lubambashi katika uwanja wa Kamarondo kwenye mechi na TP Mazembe.

Bila kusahau mjini Tunis nyumbani kwa Esperence. Pia kuna Misri nyumbani wa Al Ahly bila kusahau Asec Mimosas, Canon Younde, Horoya Guinea na kwingine kwingi. Bila saikolojia ya wachezaji nzuri, Simba atapata shida sana away games.
 
Simba wajikite kwenye ligi ya Bongo, kimataifa hata Gor Mahia ya Kenya hawawawezi
 
Umechelewa sana kuanza hii kazi ya ulozi.

Watu kama nyie mmeshindwa tayari maana tumeshaona mfano kwenye covid 19.Tumewekeza na tunajiamini tutafanya vizuri.

Mwisho nikushauri,kuwanga hadharani hivi ni aibu na si kitendo cha kiungwana
Simba wajikite kwenye ligi ya bongo, kimataifa hata gor mahia ya Kenya hawawawezi
 
Umechelewa sana kuanza hii kazi ya ulozi.

Watu kama nyie mmeshindwa tayari maana tumeshaona mfano kwenye covid 19.Tumewekeza na tunajiamini tutafanya vizuri.

Mwisho nikushauri,kuwanga hadharani hivi ni aibu na si kitendo cha kiungwana
Kama Simba ilitolewa na timu dhaifu UD SONGO. Gor mahia wataiwezea wapi?
 
Habari wadau,

Mimi mwanayanga. Ila namkubali mo kwa uwekezaji wa Simba.

Natazama sana mashindano ya CAF Champions League kila msimu. Mimi ni die hard African football fan boy. Natazama CAF Champions League kuliko UEFA.

Mashindano ya CAF ni magumu sana na yana tofaut sana na UEFA, maana ni pride sana, yaani timu zinachezea pride.

Ukiwa away hata uwe na timu kali vipi, unashambuliwa kama mwizi na kama hauko vizuri kisaikolojia unafungwa nyingi.

Simba kilichobaki iwekeze kwenye saikojiaza wachezaji, ikiwezekana wawe na mtaalamu wa kuwaongoza saikolojia.

Maana simba bila saikolojia haiwez pata hata sare mjini casablanca kwenye mechi na waydad ama raja Casablanca. Simba haiwezi pata matokeo mjini aba kwenye mechi na enyimba pale Enyimba Stadium katikati ya Igboland, Aba State, (maana wenye Enyimba ni kabila kubwa Nigeria wa Igbo na uwanja wao wa nyumbani upo kijijini kwao)

Ni sawa una mechi na Wazaramo harafu mechi unaicheza msanga ama Wakurya mechi inachezwa Tarime nyamwaga) Simba haiwez pata hata sare pale mjini Pritoria kwenye Lucas Moripe Stadium kwenye mechi na Memelodi Sundown, bila saikolojia siioni Smba ikipata hata sare pale mjini Lubambashi katika uwanja wa Kamarondo kwenye mechi na TP Mazembe.

Bila kusahau mjini Tunis nyumbani kwa Esperence. Pia kuna Misri nyumbani wa Al Ahly bila kusahau Asec Mimosas, Canon Younde, Horoya Guinea na kwingine kwingi. Bila saikolojia ya wachezaji nzuri, Simba atapata shida sana away games.
Mimi Ni shabiki wa Simba ila umeongea points tupu soka la Africa Kila timu ikiwa kwao inakua Moto Sana na Kama hampo vizuri kisaikolojia mnakula nyingi
 
Hakuna shaka yoyote ukanda huu wa Africa mashaliki hakuna team ya kuipanda simba kichwan ,team yoyote ya ukandaa huu kwa simba lazima ikae hutaki bwekaa tusikie
Daadeki😀
 
Huo ndio ukweli, mfano msimu mwaka juzi Al Ahly alipigwa kwa mkapa bila tatizo licha ya kuwa Ni team Bora kwa Africa,

CCL Ni ngumu Sana na mara nyingi tunafeli sababu ya saikolojia tu, mfano tulipotolewa na TP Mazembe pale Lubumbashi, wachezaji wangeziba masikio kelele za mashabiki na kuamua kupambana Tp Mazembe angelala hata 2- 1
 
Horoya timu aliyoenda makambo.. ilimfunga tp mazembe kwake na ikamtoa robo fainali..

Simba lile goli la mapema alilounga okwi pale congo lilitosha kabisa kumaliza mechi

Mazembe ni timu kubwa ila haijawai mtoa mtu robo fainali ama nusu fainali kwa magoli mengi kama aliyomfunga simba... sababu timu zimewekeza kwenye saikolojia wanajua wakienda pale mazembe wachezaje ili wapate matokeo.. simba alienda kizembe zembe ndio maana hakutumua chance ile ya goli la mapema kupata matokeo

Na hata msimu huu mazembe katolewa robo fainali na raja casablanca.. na mechi ya pili mazembe kamalizia kwake congo.. ila raja wamecheza kibabe sana congo na wakapata matokeo 2-1
 
Ndo hivyo Mkuu, Simba wanatakiwa kujiamini na kujenga "usugu" wa kisaikolojia hasa wawapo away, kule away mtazomewa na kuharibiwa kisaikolojia ilihali wapinzani wenu wanapewa morali kutokana na hizo kelele za mashabiki!

Kwa uwekezaji uliopo Simba Ni hasara kubwa Sana iwapo tutabaki kutamba kwenye ligi ya ndani bila kupata mafanikio kimataifa.

Zesco United Ni team hafifu na haina budget Kama ya Simba lakini mara nyingi wamefanikiwa kufika hatua za mbali kwenye CCL.

Simba must turn on international competitions rather than focusing much on local tournaments!
 
Back
Top Bottom