Simba tuache kutafuta visingizio, Kwa sasa Yanga wametuacha mbali sana

Simba lunyasi

JF-Expert Member
Joined
Sep 28, 2022
Posts
385
Reaction score
840
Miaka minne nyuma hawa utopolo walikuwa sio chochote sio lolote kwa simba, tuliwatania kila aina ya matusi na kejeli, mara bakuli fc, mara utopwinyo fc, mara kabwili fc n.k

Haya matusi na kejeli yaliwapa hasira na nguvu za kuamka kutoka usingizi wa pono, wakafanya uchaguzi kwa kuchagua viongozi wazuri wenye maono ya mpira na kiu ya mafanikio.
Hawakuishia hapo , wakaanza kufanya sajili nzuri sana tena za kimkakati, and the rest is history

Waswahili wanasema mtu mzima ukivuliwa nguo chutama. Simba tuachane na kuwekeza kwenye hamasa na propaganda, Mpira unachezwa hadharani na kila mtu anauona.
 
Wakupe Mo energy moja nakuja kulipa.

Mpira ni mchezo wa hadharani, Mhasibu wetu OKW BOBAN SUNZU wakati Yanga tunasajiri yeye alikuwa bize kutukejeri sasa tunakula matunda, wana Yanga tuna furaha tele.
 
Mangungu anatuharibia timu. Mimi binafsi hata Simba ikikutana na maji maji ya Songea naanza kwanza kuamini kuwa Simba itapigwa, ikitokea tofauti basi ni Alhamdulilah!

Sent from my SM-A042F using JamiiForums mobile app
 
Hakika
 
Rank zinatoka kwenye historia na siyo hali ya sasa..!!
Na kadiri miaka inavyozidi kwenda mbele, yale MAVUNO ya miaka ya nyuma, hayatahesabiwa, kutokana na idadi ya miaka inayohesabiwa kutoka hapa, kurudi nyuma. Hivyo, hii nafasi iliyopo Simba huko CAF, ni mavuno mazuri ya miaka iliyopita.
 
Na kadiri miaka inavyozidi kwenda mbele, yale MAVUNO ya miaka ya nyuma, hayatahesabiwa, kutokana na idadi ya miaka inayohesabiwa kutoka hapa, kurudi nyuma. Hivyo, hii nafasi iliyopo Simba huko CAF, ni mavuno mazuri ya miaka iliyopita.
Na hali ya leo itaonekana kwenye ranks siku za mbele
 
Ni kweli kabisa. Acha tu tuumie na kina Mangungu wetu. Sijui lini watatuonea huruma wajiuzulu tupate watu wapya watutoe hapa? Sijui tukawapigie magoti kuwaomba waondoke? Wanatudhalilisha sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…