Replica
JF-Expert Member
- Aug 28, 2017
- 1,681
- 8,887
Leo klabu ya Simba imefanya mkutano na waandishi wa habari kuelekea mchezo wake na timu ya Platnum kutoka Zimbabwe. Pamoja na mambo mengine, msemaji wa Simba, Haji Manara amesema wameliomba shirikisho la miguu barani Afrika kuruhusu mashabiki waingie uwanjani kwa asilimia 100, Simba wameruhusiwa kuingiza mashabiki asilimia 50 ya uwanja kutokana na janga la korona.
Manara: Tumepata barua kutoka shirikisho la mpira wa miguu barani Afrika, CAF wameridhia kwanza mechi irejeshwe saa 11 jioni, lilikuwa ni ombi letu, mwanzo ilipangwa ratiba mechi iwe saa moja kwa saa za Afrika Mashariki lakini sisi kwa kuangalia miundombinu ya Dar es Salaam, hulka za watu wa Dar na watanznia, tulipendelea mechi hii ichezwe saa 11 jioni.
Tumekuja na War in Dar kutia nguvu hii mechi, kuwapa hamasa mashabiki na wachezaji wetu, hatukuwa na nia nyingine. Wapo waliotafsiri kama vita hivi ya bunduki, hapana. ni '90 minutes battle'
Hii inapelekea tuwe na uhakika sasa wa idadi ya washabiki kufikia asilimia 100 ambayo tumeiomba kwa CAF, bado hawatujibu tujaze asilimia 100 lakini kwa sasa ni asilimia 50, wakituruhusu tutapeleka asilimia 100
Pia Manara amewananga na kuwataka waache 'viherehere' wale ambao hawaitakii mema klabu ya Simba kufuzu mashindano hayo ilhali wao wakifuzu Tanzania itakuwa na nafasi nne ya timu nne. Manara amesema hakuna namna Simba atakosa tena ubingwa mwaka huu hivyo wataendelea kuapanda ndege peke yao nafasi zisipoongezeka.