Simba: Tumeiomba CAF tujaze mashabiki uwanjani kwa asilimia 100 mechi ya Platinum. Yasema nguvu ya Simba ni mashabiki wake

Replica

JF-Expert Member
Joined
Aug 28, 2017
Posts
1,681
Reaction score
8,887
Leo klabu ya Simba imefanya mkutano na waandishi wa habari kuelekea mchezo wake na timu ya Platnum kutoka Zimbabwe. Pamoja na mambo mengine, msemaji wa Simba, Haji Manara amesema wameliomba shirikisho la miguu barani Afrika kuruhusu mashabiki waingie uwanjani kwa asilimia 100, Simba wameruhusiwa kuingiza mashabiki asilimia 50 ya uwanja kutokana na janga la korona.

Manara: Tumepata barua kutoka shirikisho la mpira wa miguu barani Afrika, CAF wameridhia kwanza mechi irejeshwe saa 11 jioni, lilikuwa ni ombi letu, mwanzo ilipangwa ratiba mechi iwe saa moja kwa saa za Afrika Mashariki lakini sisi kwa kuangalia miundombinu ya Dar es Salaam, hulka za watu wa Dar na watanznia, tulipendelea mechi hii ichezwe saa 11 jioni.

Tumekuja na War in Dar kutia nguvu hii mechi, kuwapa hamasa mashabiki na wachezaji wetu, hatukuwa na nia nyingine. Wapo waliotafsiri kama vita hivi ya bunduki, hapana. ni '90 minutes battle'

Hii inapelekea tuwe na uhakika sasa wa idadi ya washabiki kufikia asilimia 100 ambayo tumeiomba kwa CAF, bado hawatujibu tujaze asilimia 100 lakini kwa sasa ni asilimia 50, wakituruhusu tutapeleka asilimia 100

Pia Manara amewananga na kuwataka waache 'viherehere' wale ambao hawaitakii mema klabu ya Simba kufuzu mashindano hayo ilhali wao wakifuzu Tanzania itakuwa na nafasi nne ya timu nne. Manara amesema hakuna namna Simba atakosa tena ubingwa mwaka huu hivyo wataendelea kuapanda ndege peke yao nafasi zisipoongezeka.
 
Kama kujibiwa kwa barua sawa ukileta U kariakoo na Tanzania wa kudanganyana kwamba mungu anaipenda Tanzania kuliko ROMA na wakatoriki wa kule tunakula barn tu.
 
Iweje kuhusu muda wamejibu wakasahau idadi ya watu kuingia?

Sent from my TECNO F3 using JamiiForums mobile app
Barua inaweza kusema tu

Ombi lenu kuhusu muda limekubaliwa..............,...........

Kuhusu Suala la idadi ya Watu, Kamati ya Afya ya CAF inaendelea kufanya tathmini zake na Mamlaka husika zitawarejea kuhusu suala hilo lakini kwa sasa tunasimamia maamuzi ya mwisho ambayo ni nusu uwezo wa Kiwanja.

Nimekuonyesha tu mfano barua moja inavyoweza kujibu masuala mawili moja likikubaliwa lingine likawa pending
 
Naomba mikia atolewe talewa sana kwa fraha
Kweli brother kwa mikia kutolewa nilazima. Wao wenyewe wanajua wanatolewa ndio mana manara anaweweseka kila siku anakuja najipya hajiamini kabisa.Mara oooo war in dar Mara oo sisi sio timu ya wanaichi au wazalendo leo tena kaja jingine analalamika anahofia yanga tunawahujumu.ko kwa ushahidi huu wote bila Shaka yeyote Simba anatolewa, au naongopa ndugu zangu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…