Majira ya saa 1:00 usiku kwa masaa ya Afrika ya Mashariki, Mabingwa wa Nchi, Simba Sc watashuka dimbani uwanja wa Benjamin Mkapa maeneo ya Temeke, kumenyana na KMC Fc ya Kinondoni!
Machampioni hao watakuwa wakiingia uwanjani huku wakiwa na kumbukumbu ya kuibuka na ushindi wa 1-0 katika mchezo uliopita wa ligi dhidi ya Mbeya City jijini Mbeya! Simba atajaribu kushinda leo ili awese kupunguza tofauti ya point kati yake na vinara Yanga!
Wachezaji karibia wote wapo fiti kwaajili ya mtanange huo, lakini nichukue nafasi kuwakumbushia wanamichezo na wanasimba kwa ujumla, KMC sio timu ya kubeza hivyo wasiwadharau!
Je, unategemea matokeo ya aina gani? Karibu kwa ubashiri.