Simba waache uswahili je ni kweli wameshindwa kuachana na wachezaji wao kwa Staha?

Life2

JF-Expert Member
Joined
Jun 8, 2016
Posts
3,387
Reaction score
4,880
Baada ya kupewa thank you nyingi na wachezaji wake timu ya Simba ni kama wamechanganyikiwa, kuanzia Mwenyekiti wao mpaka mashabiki kila mmoja anakuja na kauli zake.

Hawana tofauti na wale wajenzi wa mnara wa Babeli lete tofali anapeleka Beleshi.

Nimepita sehemu nimekutana na kauli isiyo ya kiungwana kauli isiyo ya kimichezo kutoka kwa mmoja wa viongozi wa Simba.

Binafsi ni kauli inayoonyesha kushindwa, kukata tamaa, kuwatupia wengine lawama na kukwepa majukumu.

Huwezi kuwaita wachezaji waliopigania timu mpaka kucheza fainali kubwa Afrika Wasaliti, wote tumekua mashahidi jinsi wachezaji walivyovuja jasho kuipigania Simba.

Nisiandike sana wache nishiriki na nyie taarifa yenyewe.

 
Unataka kutueleza kitu gani?Eleza ulichokisikia huko kijiweni.Na, ukumbuke,ya kijiweni si kauli ya uongozi/timu.Acha nongwa.
 
Ulitaka asemeje..waswahili wakiambiwa ukweli wanasema unawadharau
 
Tunajenga timu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…