Komeo Lachuma
JF-Expert Member
- Oct 31, 2014
- 7,926
- 17,030
kutokana na hali ya kimashindano na maandalizi ya ligi kuu kuzidi kuwa ngumu na mwisho kuambulia pesa kidogo za mshindi wa kwanza wa Ligi kuu ya Tanzania Bara Simba ni bora ikawa inashiriki kombe moja tu la nani mtani jembe ambalo hili kila mara Simba imekuwa ikipokea si chini ya Mil 90 kwa mechi moja. hili ni wazo ambao nimeona ni bora kuwashauri Simba kuwa wawekeze zaidi kwenye kombe hili ambalo ni la mechi moja tu lakini lenye pesa nying kuliko la ligi ya vodacom. Lakini waswas unakuja kuwa kuna uwezekano mkubwa wa Yanga kususia kombe hili maana limekuwa ni sabab ya majonzi kwa vijana wa Mtaa wa Mafuriko (jangwani) ambao kila mara wanapokutana na Mnyama wamekuwa wakiambulia kipigo cha paka mwizi na hivyo kuhamishia hasira zao kwa bench la ufundi.hayo yanaonekana kama yanaweza kuja kuleta athari hapo mbeleni kwa sababu kuna uwezekano mkubwa wa Yanga kukataa kushiriki kombe hili hasa kwa kuona kuwa ni kama kuwapatia tu Simba ushindi na pesa hizo za bure .