Simba wakamatwa tena Shinyanga wakiroga

bujashi25

JF-Expert Member
Joined
Jun 17, 2013
Posts
623
Reaction score
112
Mmoja wa timu ya Simba aliyefahamika kwa jina la Rajabu Jota alikamatwa na mashabiki wa Stand United akimwaga dawa katika mlango wa kutokea wachezaji wa timu ya Stand United.

Kitendo hicho kilisababisha mashabiki wa Stand kumchapa makofi na makonde kabla ya Jeshi la Polisi kufika eneo la tukio na kumchukua mtuhumiwa.

Baada ya mchezo kuisha kocha mkuu wa timu ya Stand Mathias Lure ameeleza kufurahishwa na matokeo hayo na kuahidi kuwa ataendelea kufanya mabo makubwa katika timu yake.

Kwa upande wake kocha mkuu wa Simba Golan Kuponovic amesema Stand siyo timu ya kubeza ni timu nzuri ndiyo maana wameshinda katika mchezo huo.
​
 
Na kwa kuroga kwao ameambulia kichapo
jamaa aliyekamatwa na matunguri ya uchawi alipewa kichapo na washkaji wa stendi kisha polisi wakamzoa mpaka rumande, hili li timu kwa UCHAWI ni balaaa
 
Wanaoroga ni Simba-UKAWA. Kama mashabiki wa Stand United wangeligundua hilo, wasingemchapa makofi kwani alikuwa anawasaidia wao
 
Hii ndio Kambarage! HIVI Simba wana akili kweli?? Unaleta uchawi wa Pwani Usukumani? Au ni uchawi wa Kisumbwa toka Kahama?
au Simba alivimbiwa michembe?
 
mikia wanazidi kuumbuka kwelikweli kwa kutegemea uchawi kushinda mechi zao.....mechi ijayo wakishinda utawasikia wao ndo wameanza ligi
 
mikia wanazidi kuumbuka kwelikweli kwa kutegemea uchawi kushinda mechi zao.....mechi ijayo wakishinda utawasikia wao ndo wameanza ligi

Mkuu bujashi hebu ninong'oneze kidogo hivi mechi ijayo hii mikia mirefu fc inacheza na timu gani!!?
 
Mkuu bujashi hebu ninong'oneze kidogo hivi mechi ijayo hii mikia mirefu fc inacheza na timu gani!!?
hahaha! mikia wanalo mwaka huu...mechi ijayo wanalifuata LIBOLO FC la migambo shooting ya Tanga, naombea wakalie viwili tu halafu washindwe kuvichomoa
 
hahaha! mikia wanalo mwaka huu...mechi ijayo wanalifuata LIBOLO FC la migambo shooting ya Tanga, naombea wakalie viwili tu halafu washindwe kuvichomoa

Mikia wanatia huruma sasa, tufunge na kuwaombea angalau washinde hiyo mechi ya LIBOLO la Tanga maana tutakosa mtani mufa si mrefu.
 
Mikia wanatia huruma sasa, tufunge na kuwaombea angalau washinde hiyo mechi ya LIBOLO la Tanga maana tutakosa mtani mufa si mrefu.

mkuu makoye matale mimi Huku nshaanza kabisa ili katika zile timu 14 Za vpl iwe ya 12..nadhan mpaka hapo maombi yetu yatakuwa yamefanya kazi kabisa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…